TANGAZO


Wednesday, November 26, 2014

Harakati za uandikishwaji wananchi kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa jijini Dar es Salaam

Mwandikishaji wa kituo cha kujiandikisha  cha kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Beatrice Likundo (kulia) kilichopo kwenye Shule ya Msingi Mivinjeni jijini Dares Salaam, akimwandikisha jina leo  Mkazi wa Mtaa wa Mivinjeni, Evod Millinga kwa ajili ya uchaguzi huo.
Mkazi wa Mtaa wa Mivinjeni, Asha Bakari (kushoto), akijiandikisha leo, kwa mwandikishaji wa kituo cha kujiandikisha cha kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Beatrice Likundo kilichopo kwenye Shule ya Msingi Mivinjeni jijini Dar es Salaam.
Mkazi wa Mtaa wa Mivinjeni, Asha Bakari (kushoto), akijiandikisha leo kwa mwandikishaji wa kituo cha kujiandikisha cha kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Beatrice Likundo kilichopo kwenye Shule ya Msingi Mivinjeni jijini Dar es Salaam.
Mkazi wa Mtaa wa Mivinjeni, Evod Millinga (kushoto), akijiandikisha akionesha kitambulisho chake kwa mwandikishaji wa kituo cha kujiandikisha  cha kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa leo, Beatrice Likundo (kulia), kilichopo kwenye Shule ya Msingi Mivinjeni jijini Dar es Salaam.
Mkazi wa Mtaa wa Mivinjeni, Gilbert Katoto (kulia) akitia saini leo, mara baada ya kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali Mitaa  katika kituo cha kujiandisha cha Katakiu kwa Bea kilichopo kwenye  Mtaa wa Mivinjeni  jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwandikishaji wa kituo hicho, Isabela  Mwera.
Mkazi wa Mtaa wa Shimo la Udongo, Abdallah  Rashid Abdallah (kushoto), akitia saini leo, mara baada ya kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa leo jijini Dar es Salaam katika kituo cha polisi cha Shimo la Udongo. Kulia ni mwandikishaji wa kituo hicho, Nongaki Hassan. (Picha zote na Magreth Kinabo - Maelezo)

No comments:

Post a Comment