TANGAZO


Thursday, November 6, 2014

Berahino atajwa timu ya taifa England

Saido Berahino
Mshambuliaji wa West Bromwich Albion Saido Berahino mwenye asili ya Burundi ametajwa kwenye timu ya Taifa ya England.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21 anatarajiwa kuonekana kwenye orodha ya majina ya timu ya England katika mechi ya kimataifa ya kuwania kufuzu fainali za Euro mwaka 2016 kati England Slovenia mechi itakayopigwa Novemba 15 mwaka huu.
Berahino ambaye alizaliwa nchini Burundi tayari ameshatia wavuni magoli saba katika mechi 10 za ligi kuu ya England ambayo timu yake West Bromwich imecheza kwa msimu huu.
Timu kamili iliyotajwa na kocha England Roy Hodgson hii hapa chini

Walinda Mlango :

Fraser Forster, Ben Foster na Joe Hart

Safu ya Ulinzi:

Leighton Baines, Gary Cahill, Calum Chambers, Nathaniel Clyne, Kieran Gibbs, Phil Jagielka, Luke Shaw na Chris Smalling.

Viungo:

Ross Barkley, Michael Carrick, Stewart Downing, Jordan Henderson, Adam Lallana, James Milner, Alex Oxlade-Chamberlain, Raheem Sterling, Andros Townsend, Jack Wilshere na Theo Walcott.

Washambuliaji:

Rickie Lambert, Wayne Rooney, Daniel Welbeck na Saido Berahino.

No comments:

Post a Comment