Waandishi wa habari wakiwa kazini wakati wa mkuato huo.
Frank
Mvungi-Maelezo
MAMLAKA ya Hali ya hewa Tanzania (TMA), imedhamiria kufungua Ofisi za Kutolea huduma za
hali ya Hewa ili kupunguza ajali katika maziwa hapa nchini.
Hayo
yamesemwa leo, jijini Dar es Salaam na Meneja wa Huduma za Utabiri wa TMA Bw. Samwel Mbuya wakati wa mkutano na
waandishi wa Habari.
Mamlaka
ya Hali ya Hewa Tanzania imeona kuna umuhimu wa kujenga vituo vya kutoa huduma
za Hali ya hewa nchini katika maziwa ya Victoria,Tanganyika na Nyasa, vituo
hivi vitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza ajali kwa kuwa tutafunga vifaa vya
kisasa vya kupima hali ya hewa Alisema Mbuya.
Aidha
Mbuya amesema kuwa TMA imeendelea kuboresha huduma za utabiri wa Baharini kwa
kuweka maboya maalum katika ukanda wa bahari ya Hindi pamoja na kufungua kituo
cha hali ya hewa katika Bandari ya Zanzibar.
Mbuya
alibainisha kuwa kwa upande wa usafiri wa anga TMA imeendelea kutoa huduma
zenye kukidhi vigezo vyenye hadhi ya Kimataifa ili kuleta usalama kwa watumiaji
wa Usafiri huo nchini.
Akizungumzia
kuhusu uboreshaji wa mtandao wa vituo,Mbuya alisema kuwa hivi sasa mtandao huo
umeongezeka ikiwemo kusimikwa kwa rada mbili za hali ya hewa moja ipo katika
eneo la Bangula-Dar es salaam na nyingine iko katika hatua za mwisho huko Kiseke-Mwanza.
Pia
Mbuya aliongeza kuwa Mamlaka hiyo imefanikiwa kuongeza wigo wa usambazaji
taarifa zake hadi kufikia zaidi ya radio 40 za kijamii lengo likiwa ni
kuwafikia wananchi waliopo vijijini.
Dira
ya TMA Inalenga kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2015 Mamlaka hiyo inatoa huduma
katika viwango vya Kimataifa.
No comments:
Post a Comment