TANGAZO


Friday, October 3, 2014

Mkutano wa Nobel A.Kusini wafutwa

Dalai Lama kushoto akiandamana na marehemu Nelson Mandela
Mkutano wa washindi wa taji la Nobel unaotarajiwa kufanyika mjini Cape Town umefutiliwa mbali baada ya Afrika Kusini kukataa kumpa visa Dalai Lama.
Uamuzi huo ulifanywa baada ya washindi 14 kutishia kususia mkutano huo.
Meya wa mji wa Capetown Patricia De Lille aliunga mkono tishio hilo na kuishtumu serikali kwa msimamo huo.
Afrika Kusini imemkataza visa mara tatu katika kipindi cha miaka mitano kiongozi huyo wa kidini.
Desmond Tutu
Mkutano huo wa 14 ulipangiwa kuanza wiki ijayo ,lakini waandalizi wanasema kuwa sasa utahamishwa hadi taifa jengine.
Wanaoshiriki walipanga kusheherekea maadhimisho ya miaka 20 tangu kuisha kwa ubaguzi wa rangi mbali na kumsherehekea maremu Nelson Mandela kama mmoja ya walioshinda tuzo hilo
Dalai Lama siku ya alhamisi aliishtumu Afrika Kusini kwa kumuonea.
Imependekezwa kwamba Afrika Kusini inajaribu kujiunga na Uchina ambayo inadai kwamba kiongozi huyo wa kidini anapanga kujitenga kwa Tibet nchini Uchina.
Desmond tutu,ambaye ni mshindi wa taji la Nobel pia aliikosoa serikali ya Afrika kusini.

No comments:

Post a Comment