TANGAZO


Tuesday, October 7, 2014

Mashindano ya SHIMIWI: Habari yazidi kuchanja mbuga

Wachezaji wa mpira wa miguu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaaduni na Michezo (waliovalia jezi nyeusi) wakisalimiamana na wachezaji wa Wizara ya maji (waliovalia jezi ya kijani) kabla ya mchezo wao uliochezwa katika nyasi za uwanja wa Mazimbu mjini Morogoro. 
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaaduni na Michezo wakiomba dua kabla ya mchezo wao na timu ya Wizara ya maji kabla ya mchezo uliochezwa katika nyasi za uwanja wa Mazimbu mjini Morogoro.
Mlinda mlango wa timu ya likuwa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaaduni na Michezo Ramadhani Mtenga (kulia) akipongezwa na mlinda mlango mwenzake Idrisa Rashidi (kushoto) mara baada ya timu yao kuibuka kuwa mshindi kwa penati 3 -1 dhidi ya Wizara ya Maji.
Mwalimu wa timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaaduni na Michezo Tunge Shem akishangilia ushindi wa timu nyake dhidi ya timu ya Wizara ya Maji wakati wa mashindano ya SHIMIWI mjini Morogoro.
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaaduni na Michezo wakishangilia ushindi wa timu yao wakati wa mashindano ya SHIMIWI dhidi ya Wizara ya Maji leo mjini Morogoro. (Picha zote na Eleuteri Mangi –MAELEZO)

Habari yazidi kuchanja mbuga SHIMIWI.
NA Eleuteri Mangi-MAELEZO
06/10/2014
Hoi hoi na nderemo zimepamba moto katika viwanja mbalimbali mkoani Morogoro wakati watumishi wa umma wakioneshana utaalamu katika michezo mbalimbali wakati wa mashindano ya SHIMIWI inayoendelea mjini Morogoro.

Ndermo hizo zimeonekana Wizara ya Habari, Vijana, Utamaaduni na Michezo ilipofanikiwa kuingia hatua ya robo fainali mpira wa miguu kwa kuwatoa Wizara ya maji kwa njia ya matuta katika mchezo uliochezwa katiak nyasi za uwanja wa Mazimbu mjini Morogoro.
Mchezo huo uliisha kwa timu hizo kufungana bao 1-1 ambapo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaaduni na Michezo ndio walikuwa wa kwanza kuliona lango la Wizara ya Maji dakika ya 21 kipindi cha kwanza kwa goli lililofungwa na James Mapepe wakati goli la kusawazisha la Wizara ya Maji lilifungwa kipindi cha pili na mchezaji Alifa Ismail katika dakika ya 40 ya mchezo.

Baada ya dakika 60 za mwamuzi wa mchezo huo Baraka Rashidi, timu hizo zilikuwa na goli moja kila mmoja hivyo mwamuzi huyo kwa kufuata kanuni na taratibu za mashindano hayo aliamuru matuta yapigwe ili apatikane mshindi.

Mlinda mlango wa timu ya likuwa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaaduni na Michezo Ramadhani Mtenga ndiye aliyeibuka kuwa shujaa wa mchezo kwa kupangua penati moja na kuipa timu yake ushindi wa penati 3 -1 dhidi ya Wizara ya Maji.


Mwamuzi wa mchezo huo alisaidiana na washika vibendera Erick Joseph na Ramadhani Sadick wakati kamisaa wa mchezo huo alikuwa Godifrey Evance wote wanatoka kituo cha kukuza vipaji vya michezo cha Twalipo Youth Foundation cha mjini Morogoro.

No comments:

Post a Comment