TANGAZO


Monday, October 13, 2014

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, atembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa wa NSSF Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Idd, akijadili jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhan Dau (watatu kushoto), alipotembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa zinazojengwa na shirika hilo, Kijichi, Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo. (Picha zote na Mpigapicha Wetu)
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau, akimuonesha Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (kulia kwake), baadhi ya nyumba zinazojengwa na shirika hilo, Kijichi, Dar es Salaam leo. Kushoto kwa Dk. Dau ni Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo.

Makamu wa pili Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (wa pili kulia), akiwasikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhan Dau (kulia kwake) na Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo, wakati wakimuonesha baadhi ya nyumba za kisasa zinazojengwa na shirika hilo, Mtoni Kijichi, Dar es Salaam leo.

Makamu wa Pili Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (wapili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhan Dau (kulia) na Meneja Miradi wa shirika hilo, Mhandisi John Msemo, wakimwangalia mke wa Makamu wa pili wa Rais, Mama Asha Seif, wakati akionesha michoro ya nyumba ziliomvutia, walipotembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa, Kijichi Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment