TANGAZO


Sunday, October 12, 2014

Kimbunga kikali chawaua watu 6 India

Hudhud
Watu sita wameripoti kufariki nchini India baada ya kimbunga chenye nguvu nyingi kwa jina 'Hudhud' kupiga eneo la pwani ya India kikiwa na upepo unaovuma kwa kasi ya hadi kilomita 180 kwa saa.
Utawala unasema kuwa kati ya masaa matano na sita yanayokuja yatakuwa muhimu.
Watu 350,000 waeondolewa kutoka maeneo ya Andhra Pradesh na Orissa.
Vituo vya huduma za dharura vimefunguliwa huku vikosi vya usalama vikiwekwa kwenye hali ya tahadhari.
India Cyclone
Mwandishi wa BBC katika eneo hilo anasema kuwa India imepoteza kwa kiwango kikubwa huduma zake za dharura.
Katika ripoti yake ya hivi karibuni Idara ya hali ya hewa nchini India imesema kuwa hali katika eneo la baharini itakuwa mbaya katika eneo la kazkazini mwa Andhra Pradesh na katika pwani ya Orissa.
Pia imeonya kuwa kimbunga kikali cha hadi mita mbili katika maeneo ya chini ya Visakhpatnam ,vijayanagram na Srikakulam.
Kimbunga kikali mnamo mwaka 1999 kiliwaua watu 10,000 katika eneo la Orissa.

No comments:

Post a Comment