TANGAZO


Tuesday, October 14, 2014

Kim Jong-un aonekana hadharani


Picha iliyopigwa katika gazeti la Rodong Sinmum Okta 14, 2014 ikimwonyesha kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un akikagua eneo jipya la ujenzi wa makaazi mjini Pyongyang

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kwa mara ya kwanza ameonekana hadharani tangu Septemba 3, limesema shirika la habari la nchi hiyo.
Shirika la habari la Korea Kaskazini, KCNA limesema Jumanne kuwa Bwana Kim ametoa maelezo katika eneo jipya lililojengwa kwa ajili ya makaazi ya wanasayansi.
Gazeti la Rodong Sinmun limechapisha picha kadha za Bwana Kim akitembea kwa kutumia mkongojo wakati akikagua eneo hilo.
Kutoonekana kwa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 32 kulisababisha taharuki juu ya afya yake.
Baadhi ya wachunguzi wanasema Bwana Kim atakuwa anaumwa ugonjwa wa jongo au matatizo katika maungio ya nyonga yake. Wengine wamehoji hata kama ana udhibiti wa Ikulu.
Gazeti la Korea Kaskazini la Rodong Sinmun limekuwa na picha kadha zinazosemekana kuwa za ziara ya Kim Jong-un.
Bwana Kim alipigwa picha akitumia mkongojo katika nyingi ya picha hizo wakati akikagua eneo la makaazi.
Kim Jong-un alichukua madaraka baada ya kifo cha baba yake, Kim Jong-il, Desemba 2011 na mara moja alitangazwa kuwa mkuu wa chama, serikali na jeshi.

No comments:

Post a Comment