TANGAZO


Friday, October 10, 2014

GODTEC yasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana

Meneja wa POSO Kanda ya Ziwa Bw. Emmanuel  Kisamba (kushoto) akitoamaelezo kwa mwananchi aliyetembelea banda la Kampuni ya GODTEC katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ambapo Maonyesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayofanyika mkoani humo kuelekea Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na Kumbukumbu ya Miaka 15 ya Kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Nyerere.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa PAFRI Bw. Boniphace Alex akitoa maelezo namna ya jiko lilotengenezwa na Kampuni yake linavyofanya kazi, kwa vijana waliotembelea banda la Kampuni ya GODTEC katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ambapo Maonyesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayofanyika mkoani humo kuelekea Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na Kumbukumbu ya Miaka 15 ya Kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Nyerere.Katikati ni Afisa Uhusiano wa Bega kwa Bega Microfinance Bibi. Dorcas David Mlapa na Afisa Mtendaji Mkuu wa PAFRI Bw. Boniphace Alex
Baadhi ya wafanyakazi wa GODTEC na Bega kwa Bega Microfince wakitoa huduma katika banda lao wakati wa Maonyesho katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ambapo Maonyesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayofanyika mkoani humo kuelekea Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na Kumbukumbu ya Miaka 15 ya Kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Nyerere. (Picha zote na Frank Shija, Tabora)

Na Jonas Kamaleki- Tabora
Kampuni ya Godtec (T) Limted ya jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imewawezesha vijana kufungua na kumiliki makampuni yao kwa ajili ya kujiajiri na kuajiri vijana wengine.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Kituo cha Huduma kwa Kanda ya Ziwa  (POSO) ambayo ni moja ya bidhaa ya Godtec, Bwana Emmanuel Kisamba wakati wa Maonyesho ya Wiki yaVijana yanayofanyika kitaifa mkoani Tabora.

Kisamba aliongezakuwa kupitia huduma hiyo Vijana wameunganishwa na kutengeneza Kampuni ya huduma za kifedha ya Bega kwa Bega Microfinace Limted ambayo inamilikiwa na vijana wenyewe na kupitia Kampuni hiyo vijana wanapata fursa kukopeshwa mitaji kwa ajili ya shughuli zaujasiriamali.

Amezitaja kampuni zilizoanzishwa chini ya utaratibu huo kuwa ni pamoja na Consultancy in Africa (COAFRI) na Power in Africa (PAFRI),Agri-Business, Active Sales and Marketing zenye makao yake jijini Mwanza.
Amesema kuwa majukumu ya kamapuni hizo ni kuwaelimisha vijana ili wajitambue na kutambua fursa zilizowazunguka nakuzitumia ipasavyo, kuwawezesha vijana kufungua makampuni yao na kuwashauri vijana katika miradi wanayotaka kuanzisha.

Mengine ni pamoja kuwasadia vijana katika kuandika maadiko ya miradi endelevu nakutoa ushauri jinsi ya kufanya biashara endelevu kwa sasa na kwa ajili ya vizazi vijavyo.

“Tunatoa mikopo kwa makampuni ya vijana na kwa kijana mmoja mmoja”, amesema Bwana Kisamba. 

Katika mikopo hiyo, dhamana ni hisa za kampuni inayotaka kukopa. Amefafanua kuwa kila kampuni inabidi inunue hisa kwenye Bega kwa Bega Microfinance Company Limited ambayo itafanya kampuni lengwa kupata faida zinazotokana na Bega kwa Bega ikiwemo na kukopesheka.

Meneja huyo alisema kuwa zipo aina tatu za mikopo ambazo alizitaja kuwa ni Anzisha, mkopo unofikia hadi shilingi milioni 5, Imarisha, unaofikia milioni 10 na Wekeza ambao kima cha juu ni milioni 50. Mikopo hii yote ina riba nafuu sana,wastani wa asilimia 10 kwa mwaka, ikilinganishwa na taasisi nyingine za kifedha nchini.
Hadi sasa jumla ya makampuni manne yameshakopeshwa na Bega kwa Bega. Meneja Emmanuel Kisamba aliyataja makampuni hayo kuwa ni COAFRI, PAFRI, Active Sales and Marketing pamoja na Agri-business. Yote haya yamekopeshwa jumla ya shilingi milioni 22.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa COAFRI Bw. Ghai Edward vijana watimie fursa inayopatikana kupitia Godtec na washirika wake kwani na kubainisha kuwa ujasiri na utayari wake baada ya kupata elimu kutoka kwa maafisa wa Godtec ameweza kuanzisha kampuni yake na kuajiri watu wengi hivyo amewataka vijana wasibweteke badala yake wathubutu kwa kuanzisha makampuni.

Ghai ameongeza kuwa kwa kijana akithubutu kujiari atakuwa amepunguza tatizo la ajira kwake mwenyewe lakini pia atakuwa amewezesha kuongeza ajira kwa vijana.

No comments:

Post a Comment