TANGAZO


Thursday, October 2, 2014

China yamuunga mkono Leung


Wengi wa waandamanaji ni wanafunzi wanamomtaka kiongozi wa Hong Kong kujiuzulu

China imetangaza kuunga mkono Kiongozi Mkuu wa Hong Kong, C Y Leung, anapokabiliwa na maandamano makubwa ambayo yamedumaza shughuli katika eneo kubwa la mji huo.
Wanafunzi wametisha kuanza kupiga kambi baadhi ya majengo ya Serikali iwapo kiongozi huyo hatajiuzulu ifikapo leo jioni.
Katika tahariri ya ukurasa wa mbele katika gazeti la kila siku la Kikomunisti Serikali inamuunga mkono kikamilifu na inamwamini na kuridhika na kazi yake.

Wamnempa hadi mwioshoni wa Alhamisi kufanya hivyo la sivyo wavamie majengo ya serikali

Serikali ya China pia ilionya kuwa lazima sheria na utangamano vidumishwe nchini humo au ghasia zitasambaa kila mahali.
Wandamanaji wanaendelea kushinda na kukesha katika maeneo muhimu hapo jijini kama vile pande mbili za bandari ya Hong Kong, kama hatua ya kuitisha Demokrasia zaidi.

Wanasema China inawakandamiza kwa kutaka kuwakagua wanasiasa wa Hong Kong kabla ya uchaguzi wa 2017

Idadi ya waandamanaji ni ndogo kuliko ilivyokuwa siku zilizopita lakini idadi hiyo huongezeka na kupunguka kulingana na muda.
Serikali ya China imemuunga mkono bwana Leung kwa vile alivyokabiliana na hali Hong Kong na pia kup[ongeza polisi kwa namna wanavyokabili maandamano ya maelfu ya watu mjini humo.
Wengi wamekerwa na tamko la China kuwa lazima wanasiasa wenye nia ya kuwania nafasi mjini Hong Kong lazima wakaguliwe na serikali ya China kwa sababu ya uchaguzi utakaofanyika mwaka 2017.

China imeunga mkono polisi kwa namna walivyokabiliana na waandamanaji

Wananchi wa eneo hilo wanasema China haistahili kuingilia siasa zake na wataendelea kuandamana hadi kiongozi wa jimbo hilo atakapoondoka mamlakani.
Serikali imetyaka waandamanaji hao kusitisha maandamano yao ikilaani ghasia na vurugu

No comments:

Post a Comment