TANGAZO


Friday, October 10, 2014

Amref Health Africa Tanzania yachangisha sh.bilioni 1.9 kusomesha wakunga ili kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua


Makamu wa Rais Dk.Mohammed Gharib Bilal akihutubia katika hafla ya chakula cha hisani kwa ajili ya kuchangia mfuko wa kampeni ya Jitolee kwa ajili ya akina mama wa Afrika iliyofanyika Oktoba-9-2014 Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kimataifa ya Amref Health Africa, Omari Issa, akizungumza katika mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Amref Health Africa Dk.Teguest Guerma 
akizungumza katika hafla hiyo. (Imeandaliwa na mtandao wa ww.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa Tanzania, Festus Ilako, akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kimataifa ya Amref Health Africa, Omari Issa (kulia), akimkabidhi zawadi Makamu wa Rais Dk.Mohammed Gharib Bilal, ambaye alikuwa ni mgeni rasmi kwenye hafla hiyo.
Naibu Mkurugenzi wa Amref  Health Africa, Dk.Rita Noronha, 
akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla hiyo.
Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti cha udhamini wa kampeni hiyo, Mkurugenzi wa ITV na Radio One, Joyce Mhavile.
Makamu wa Rais Dk.Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti cha udhamini wa kampeni hiyo, Mmiliki wa mtandao wa Jamii Forum, Mike Mckee.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kimataifa ya Amref Health Africa, Omari Issa (wa pili kushoto), akimkabidhi zawadi mbalimbali Mkurugenzi Mkuu wa Amref Africa Dk.Teguest Guerma  kutokana na mchango wake ndani ya AMREF. Kulia ni Dk.Amos Nyirenda kutoka Amref Health Africa Tanzania na kushoto ni Ofisa Msisimazi wa Amref Health Africa, Noerime Kaleeba, Ph.D kutoka Chuo Kikuu cha Makerere Shule ya Afya ya Jamii nchini Uganda.
Ofisa Msisimazi wa Amref  Health Africa, Noerime Kaleeba, Ph.D kutoka Chuo Kikuu cha Makerere Shule ya Afya ya Jamii nchini Uganda, akipongezana na Mkurugenzi Mkuu wa Amref Africa Dk.Teguest Guerma.
Dada wa Jamii ya Kimasai Tainoi Kayu Moringe kutoka Kilindi Wmkoani Tanga, aliyesomeshwa na taaluma ya uuguzi Amref Health Africa kwa ajili ya kusaidia huduma za afya ya mama na mtoto wakati akijifungua akizungumza katika mkutano huo.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo.

Wageni waalikwa wakiserebuka wimbo wa mama ulioimbwa na mwanamuzi Christian Bela wa Bendi ya Malaika.
Wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo.
Ukumbi wa Hoteli ya Serena ukiwa nyomi kama picha inavyojieleza. Pig up Amref Health Africa.
Wafanyakazi wa Amref  Health Afrika Tanzania wakitoa burudani ya nyimbo mbalimbali za kuhamasisha kampeni hiyo.


Dotto Mwaibale
AMREF Health Africa Tanzania imefanikiwa kuchangisha sh.bilioni 1.9 kwa ajili ya kusomesha wakunga ili kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
Hayo yalielezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Kimataifa ya Amref Health Africa, Omari Issa, katika hafla ya chakula cha hisani kwa ajili ya kuchangia mfuko wa kampeni ya Jitolee kwa ajili ya akina mama wa Afrika iliyofanyika Dar es Salaam jana.

"Sisi Amref Health Africa tuliiona changamoto hii nakuanzisha kampeni hii ili kuokoa maisha ya mama na mtoto wakati wa kujifungua kwani kila siku wakina mama kati 22 hupoteza maisha wakati wa kujifungua" alisema Issa.

Makamu wa Rais Dk.Gharib Bilal ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo alisema upungufu wa wakunga nchini umechangia kwa kiasi kikubwa kuwafanya akina mama kupoteza maisha wakati wa kujifungua.
"Katika maeneo mengi ya Afrika hasa vijijini hupungufu huu wa wakunga ni mkubwa sana hivyo jitihada hizi zinazo fanywa na hawa wenzetu wa Amref Health Africa zinapaswa kuungwa mkono na kila mpenda maendeleo" alisema Bilal.

Alisema kwa huko vijijini inakuwa vigumu kwa akina mama kupata huduma za afya wakati wakiwa wajawazito na hadi wakati wa kujifungua na kama huduma hizo zingalikuwepo, uwekano wa akina mama kujifungua salama ungalikuwa mkubwa na hata kupunguza vifo vya watoto wachanga.
Dk. Bilal alitumia fursa hiyo kuishukuru Amref Health Afrika  kwa kushiriki umma wa watanzania ili nao wajitokeze katika kuchangia kampeni hiyoya kujitolea  kwa ajili ya akina mama wa Afrika.

Alisema Serikali peke yake haiwezi kutoa elimu kwa wakunga wanaohitajika kwani kampeni hii inalenga kuongeza wakunga pamoja na kuwapa taaluma ya kazi hiyo ili waweze kufanyakazi vizuri na kwa ufanisi.
Alisema serikali ya Tanzania kwa dhati kabisa inatambua jambo hilo na inajitahidi kadri inavyowezekana katika kusaidia jambo hilo ambalo ni muhimu.
Dk.Bilal katika kuonesha anaunga jitihada hizo za Amref Health Afrika na za kukabiliana na vifo vya akina mama wakati wakijifungua alichangia sh.milioni 10 kwa ajili ya kampeni hiyo.

Naibu Mkurugenzi wa Amref  Health Africa, Dk.Rita Noronha alisema Amref Health Afrika imelenga kuwawezesha wakunga 3,800 ifikapo mwaka 2016 katika Tanzania na 15,000 kwa Afrika nzima.
Dk.Noronha alitoa mwito kwa kila mdau anayeguswa na jambo hilo kuendelea kuchangia kampeni hiyo kwani bado kunamahitaji makubwa ya kusaidia kundi hilo ambapo ni muhimu sana katika ustawi wa taifa lolote duniani.(Imeandaliwa na mtandao wa ww.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

No comments:

Post a Comment