TANGAZO


Friday, October 31, 2014

Dk. Gharib Bilal: Serikali kuendelea kuboresha huduma za Afya kwa wananchi

Makamu wa Rais Dk. Mohamed  Gharib Bilali (watatu kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa Sekta ya afya nchini mara baada ya kufungua Kongamano la wadau  hao leo jijini Dar es Salaam. Wengine kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Seif Rashid.
Makamu wa Rais Dk. Mohemed  Gharib Bilali akiwa kwenye picha ya pamoja  na Waziri wa Afya na ustawi wa Jamii  Dk Seif Rashid leo Jijini Dar es salaam wakati wa Kongamano la wadau wa  Sekta ya Afya lililofanyika leo Jijini Dar es  salaam. (Picha zote na Frank Mvungi-MAELEZO_Dar es Salaam)
Baadhi ya Wadau wa Kongamano la wadau wa Sekta ya Afya wakiwa wanamsikiliza mgeni  rasmi ambaye ni makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilali (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo leo jijini Dar es Salaam.

Na Frank Mvungi-MAELEZO
SERIKALI imesema itaendelea kuboresha huduma za afya hapa nchini kuanzia ngazi ya Zahanati  hadi Hosipitali za Rufaa zote nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata matatibu bora na yanayoridhisha.
Kauli hiyo imetolewa  leo jijini Dar es salaam na Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilali wakati akifungua Kongamano la wadau wa Afya nchini.

Amesema kuwa Serikali inayo dhamira ya dhati katika kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anapata huduma bora za afya ili apate muda mzuri wa kuchangia shughuli nyingine za maendeleo akiwa mzima.

Dkt. Bilali ameongeza kuwa Serikali itaendelea kutoa motisha kwa watumishi wa Sekta ya afya ili waendelee kutoa  huduma bora za afya kwa wananchi.

Kwa upande wake Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid amesema Tanzania ni moja kati ya nchi nne barani Afrika zilizoweza kufikia lengo namba 4 la malengo ya millennia katika utoaji wa huduma bora za afya.

Amesema kuwa hatua imefikiwa baada ya Wizara hiyo kuamua  kuanzisha idara maalum itakayohusika kuangalia ubora wa huduma zinazotolewa hapa nchini ili kuongeza tija katika Sekta ya Afya kwa kuwapa Wananchi huduma bora zinazokidhi vigezo.

Ameongeza kuwa kwa wale wanaofanya vizuri katika kutoa huduma za Afya watatambuliwa kwa mchango wao katika kutoa huduma bora.
Dkt. Rashid ametaja vigezo vinavyotumika katika kuwapata watoa huduma za afya kuwa ni kutoa huduma inavyotakiwa,kutumia utaalamu sahihi katika kutoa huduma hiyo na kuzingatia viwango vilivyowekwa katika kutoa huduma za afya.
Aidha Dkt.  Rashid ametoa wito kwa wananchi kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) ili waweze kunufaika na huduma zinazotolewa  kupitia mfuko huo kwa lengo la kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma bora za afya.

Kongamano la wadau wa  Sekta ya Afya limehusisha wadau zaidi ya 300 kutoka katika Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za Kiserikali na linafanyika kwa muda wa siku mbili ambapo baadhi ya wadau walitambuliwa kwa kutoa huduma bora za Afya ni kama vile Hosipitali ya Rufaa Mbeya,KCMC,  na Bugando.


Ujasiriamali na Miradi ya Uzalishaji mali Chachu ya Vijana kuachana na matumizi dawa za kulevya

Baadhi ya washiriki walioudhuria uzinduzi huo wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana wakati wa uzinduzi wa Program maalum kwa Vijana iliyoandaliwa na kituo cha MAA MEDI.
Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC,Rukia Mtingwa wa kwanza kushoto akimkabidhi  hundi yenye thamani ya shilling milioni 116,952,000 Mkurugenzi wa Kituo cha MAA MEDI bwana Furaha Levilal wa kwanza kulia katika uzinduzi wa program maalum ya Vijana.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya  Maendeleo ya Vijana Bwana James kajugusi  akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC, Rukia Mtingwa alipokuwa akizindua Programu Maalumu kwa Vijana itakayotolewa Kituo cha MAA MEDI.
Meneja wa Miradi kutoka kituo cha MAA MEDI bwana Albany James akiongea na waandishi wa habari katika uzinduzi wa programu maalum kwa Vijana iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya  Maendeleo ya Vijana Bwana James kajugusi  akizungumza na waandishi wa habari, alipokuwa akizindua Programu Maalumu kwa Vijana itakayotolewa Kituo cha MAA MEDI.

Profesa Kikwete Mgeni rasmi uzinduzi Ujenzi Kituo cha Michezo Kindongo Chekundu

Rais Profesa Jakaya Kikwete

Na Mwandishi wetu_MAELEZO-Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Profesa Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa kituo cha michezo katika eneo la Kidongo Chekundi  jijini Dar es Salaam.

Kituo cha michezo kinajengwa kwa ufadhili wa Klabu ya Sunderland kwa kushirikiana na Symbion Power na Serikali ya Tanzania.

Shehere hizo zinatarajiwa kesho asubuhi (Jumamosi tarehe 1 Novemba 2014) kuanzia majira ya saa mbili asubuhi.

Kwa mijbu wa taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es salaam na Mwakilishi wa Symbion nchini Julie Foster , sherehe hizo pia zitahudhuriwa na Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella E. Mukangara, Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Sunderland ya Nchini Uingereza Bi. Margaret Byrne na  Afisa Mtendaji Mkuu wa Symbion Power Bw. Paul Hinks

Taarifa hiyo imeongeza kuwa pamoja na uzinduzi wa ujenzi huo Rais Kikwete atapanda mti kwenye eneo hilo, akisaidiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Sunderland AFC Bi. Byrne, Mkurugenzi wa Biasharawa klabu hiyo Gary Hutchinson, na Afisa Mtendaji Mkuu wa Symbion Power  Bw. Hinks.


Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza ya Barclays, Sunderland AFC inatoa usaidizi wa kiufundi na utendaji katika uendelezaji wa mradi wa mpira wa miguu, ambao ni wa kwanza na wa aina yake nchini humu, utakaohakikisha  maelfu ya vijana wananufaika kutokana na mtazamo wa pamoja wa kuchanganya mpira wa miguu, elimu na ushiriki wa jamii, ili kupata ujuzi na utaalam wa Sunderland AFC.

Emirates Start Second Service to Dar es Salaam

Emirates Plane 
DAR ES SALAAM, TANZANIA
31 OCTOBER 2014 
EMIRATES, a global connector of people and places, has started its second service between Dubai and Dar es Salaam with the arrival this past weekend of the first flight of the new five times weekly frequency.

The new fives times weekly service complements Emirates’ existing daily operation between the two cities, and is expected to further boost inbound and outbound passenger traffic and cargo flows between Tanzania and Dubai, and Emirates’ extensive worldwide network.

“Dar es Salaam is an important destination in our east African network. In our last financial year we carried over 180 000 customers on the route and this second service is expected to further boost trade and tourism growth, and will also offer our customers more choice and convenience from Tanzania to Dubai and onward to Europe, the United States, India and the Fast East, as well as other destinations across Emirates extensive global network,” said Khalid Al Zarouni, Emirates Country Manager for Tanzania.

“This second service also makes Dar es Salaam the second destination in East Africa, after Nairobi, to have more than a daily frequency,” he added.

The new flight is operated with an Emirates A330-200, in a three class configuration with 12 seats in First Class, 42 in Business Class and 183 in Economy Class, adding a total of 2370 seats and up to 170 tons of cargo capacity a week on the route. Emirates customers will enjoy cuisine prepared by gourmet chefs and the world famous services from Emirates multi-national cabin crew, including Tanzanian nationals. Customers in all three classes enjoy generous baggage allowances, with 50 kg in First Class, 40kg in Business Class and 30kg in Economy Class.

The service operates on a Monday, Tuesday, Wednesday, Saturday and Sunday. It departs Dubai as EK727 at 1655hrs and arrives in Dar es Salaam at 2150hrs. The return flight EK728 departs Dar es Salaam at 2330hrs and arrives in the Dubai the next morning at 0620hrs.

Mambo ya Skylight Band Thai Village Masaki jijini Dar es Salaam


DSC_0159
Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar huku akisindikizwa na waimbaji wenzake kutoka kushoto ni Digna Mbepera, Joniko Flower a.k.a Baba lao, Sony Masamba pamoja na Sam Mapenzi.
DSC_0007
Aneth Kushaba sambamba na Digna Mbepera wakiwapa raha mashabiki wao (hawapo pichani) kwenye show zao za kila Ijumaa ndani ya ukumbi wa maraha wa Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0012
Kifaa kipya cha Skylight Band, Bela Kombo akitoa burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo ndani ya ukumbi wa Thai Village Ijumaa iliyopita.
DSC_0024
Kutoka kushoto Bela Kombo, Hashim Donode na Digna Mbepera wakiporomosha burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita ndani ya uwanja wao wa nyumbani Thai Village.
DSC_0057
Binti mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni Digna Mbepera kwenye hisia kali za muziki wa Live kwa mashabiki wa Skylight Band ndani ya ukumbi wa Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0026
Burudani ikiendelea.
DSC_0109
Hapa mashabiki wakizirudi ngoma za bendi hiyo.

Benki ya Exim katika Maonesho ya Wiki ya Viwango yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS)

exi
Ofisa Mauzo wa Benki ya Exim Tanzania, William Kikoti (wa pili kushoto), akimkaribisha Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw. Odilo Majengo (kulia), katika banda la benki hiyo wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Viwango yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam Jumatano. Waliopo katika banda hilo ni Mkuu wa Matawi wa Benki ya Exim, Bi. Elizabeth Majengoh (kushoto) na wafanyakazi wengine wa benki hiyo. 
unnamed1
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw. Joseph Masikitiko (kushoto), akifurahia jambo wakati akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Matawi wa benki ya Exim, Bi. Elizabeth Majengoh (wa pili kulia), juu ya huduma na bidhaa zitolewazo na benki hiyo, alipotembelea banda la benki hiyo katika Maonyesho ya wiki ya viwango yaliyoandaliwa na TBS na kufanyika katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam Jumatano. Pamoja nao ni Mkuu wa Matawi wa benki hiyo Agnes Kaganda (wakwanza kushoto) na wafanyakazi wengine wa benki hiyo. 
unnamed2
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw. Joseph Masikitiko (kulia), akiwasalimia wafanyakazi wa Benki ya Exim alipotembelea banda la benki hiyo katika Maonyesho ya Wiki ya Viwango yaliyoandaliwa na TBS na kufanyika katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam Jumatano. 
unnamed4
Ofisa Mauzo wa Benki ya Exim, Bw. William Kikoti, akifafanua juu ya bidhaa na huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo kwa baadhi ya washiriki waliohudhuria maonyesho ya wiki ya viwango yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam Jumatano. Wengine ni wakuu wa watawi wa benki hiyo Bi. Elizabeth Majengoh (wapili kushoto) na Bi. Agnes Kaganda (aliyekaa wakwanza kulia). (Picha zote na mpiga picha wetu)

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira yamaliza ziara yake katika Mgodi wa Buzwagi

unnamed
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Ummy Mwalimu akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira. Wa kwanza kulia ni Mh. James Lembeli Mwenyekiti wa Kamati hiyo.
unnamed1
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Ummy Mwalimu (katikati) akiambatana wajumbe wa Kamati katika ziara ya kukagua bwawa la kuhifadhia maji katika mgodi wa Buzwagi.
unnamed2
Pichani ni ujenzi wa awamu ya pili wa Kituo cha Afya cha Mwendakulima kinachojengwa na Mgodi wa Buzwagi kwa ajili ya kuwasogezea wananchi huduma bora za afya.
unnamed3

Baadhi nyumba zitakazotumiwa na waganga na wauguzi wa kituo cha afya cha Mwendakulima pindi kituo hicho kitakapoanza kutumika.

TFF yataka jezi mpya za soka Tanzania

Timu ya Taifa ya Tanzania ikiwa katika jezi zake za awali za bluu iliyokolea na alama za njano na nyeusi na kijani
Shirikisho la soka Tanzania, TFF, limesema linakaribisha wabunifu watakaobuni mwonekano wa jezi mpya za timu ya taifa kwa mechi za nyumbani na ugenini.
Hata hivyo sharti la ubunifu huo lazima uzingatie rangi za bendera ya taifa ambazo ni kijani, njano, nyeusi na bluu.
Wakati tangazo hili likitolewa na TFF, tayari uongozi mpya chini ya rais wake Jamal Malinzi umebadili jezi zinazotumiwa katika mechi za timu ya taifa, Taifa Stars, kutoka zile zilizozoeleka na mashabiki na Watanzania wote hadi jezi mpya zinazolalamikiwa na mashabiki wengi kuwa hazina mvuto na hazionyeshi rangi halisi ya bendera ya taifa la Tanzania.
Jezi mpya ya timu ya taifa ya Tanzania, ambayo nayo inatakiwa kubadilishwa
TFF ilipoamua kutumia jezi mpya zinazotumika sasa haikuwashirikisha wabunifu wa mavazi kuhusu jezi mpya ya timu ya taifa na badala yake ikaja na jezi ambayo imekuwa ikilalamikiwa na mashabiki kuwa haina mvuto na haiwakilishi rangi halisi za bendera ya taifa, huenda ndio maana safari hii wametoa tangazo hilo.
Mbunifu atakayeshinda atapata zawadi ya shilingi milioni moja za Kitanzania sawa na karibu dola mia saba za Kimarekani kwa atakayebuni jezi ya kuchezea mechi za nyumbani na vile vile mshindi atakayebuni jezi za kuchezea mechi za ugenini naye atapata kiasi kama hicho cha fedha.
Jezi ya sasa ina rangi ya samawati na bluu nyeusi.

Pinda atakaTanzania ijitegemee

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda
Suala la baadhi ya wafadhili wa Tanzania kubana au kuchelewesha fedha walizoahidi kusaidia bajeti ya nchi hiyo kumeendelea kuiumiza serikali.
Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda, amesema umefika wakati sasa kwa Tanzania kujitegemea kwa mapato ya ndani kwa asilimia 100 badala ya kutegemea wahisani ambao amedai wanakuwa na maslahi yao katika kusaidia.
Hivi karibuni wahisani wamesitisha kutoa fedha hizo kuishinikiza Tanzania kuchukua hatua dhidi ya upotevu wa mabilioni ya fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania katika mazingira yanayodaiwa kuwa ya rushwa.
Kiongozi huyo mwandamizi wa serikali ya Tanzania ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kurejea kutoka ziara ya ughaibuni ambako alihudhuria mikutano katika nchi mbali mbali akishughulikia masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na uwekezaji.
Japokuwa Waziri Mkuu Pinda hafafanui kwa nini serikali haichukui hatua za haraka kukamilisha uchunguzi wa upotevu wa takriban dola milioni 120 kutoka Benki Kuu ya Tanzania katika mazingira yanayodaiwa kugubikwa na rushwa kubwa, amesema wahisani hao wasingeisumbua Tanzania kama ingekuwa inajitegemea asilimia 100 kutokana na mapato ya ndani ya nchi.
“Ukishakuwa tu ni mtu ambaye unaonekana wewe bila wao taabu, ndiyo shida inaanzia hapo.Ndiyo maana wakati mwingine inabidi kusema bwana sisi tujitahidi, TRA huyu huyu twende naye akiweza kuongeza zaidi kidogo basi tutamshukuru sana.
First and foremost tumtumie yeye na tuone hiki kidogo tunachokipata kutoka TRA tunavyoweza kukitumia vizuri zaidi kutupunguzia matatizo yetu. Kama zikija hizo nyingine well and good lakini si option ambayo unasema inakupa faraja kubwa sana. kwa sababu anything jambo lolote likitokea wanabana tu, halafu matokeo yake inakuwa ovyo sana katika shughuli zenu za maendeleo,” alieleza Bw Pinda.
Ingawa kauli yake haitapunguza maumivu ya wananchi wanaosubiri huduma na utekelezaji wa miradi ambayo ilishapangwa, pia ni vigumu kufanikisha jambo analolisema kwa muda mfupi.
Waziri Mkuu Pinda alipoongea na BBC hivi karibuni alikiri kwamba madai hayo ya utoroshaji wa fedha ni jambo linaloitia doa serikali ya Tanzania.
Swala hilo linaonyesha kuiumiza kichwa serikali wakati hasa kutokana na shughuli nyingi za maendeleo kuchelewa au kukwama, huku ikijikuta ikiwa haina njia nyingine ya haraka kurekebisha hali ya mambo.
Hata hivyo Waziri wa Fedha na Uchumi, Saada Mkuya Salum, akizungumza mjini Dar es Salaam amesema baadhi ya wahisani wamekwishatoa fedha na mazungumzo yanaendelea na waliobaki.
Ripoti ya uchunguzi unaofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ambayo imekuwa ikifanya kazi hiyo kwa miezi kadhaa inasubiriwa kwa hamu ili ibainike endapo kulikuwa na hila katika kuchomolewa fedha zilizokuwa zimewekwa kwenye akaunti maalum katika Benki Kuu ya Tanzania kusubiri usuluhishi wa suala la kibiashara umalizike.

Kiwango cha kalori katika pombe kitajwe

Wataka pombe ionyeshe kiwango cha kalori kupunguza vitambi na unene wa kupitiliza
Pombe inatakiwa kuwa na nembo inayoonyesha kiwango cha kalori au kipimo cha joto litolewalo na chakula ili kupunguza vitambi au unene wa kupita kiasi.
Madaktari wa afya ya umma, wameonya kuwa glasi kubwa ya mvinyo inaweza kuwa na kiasi cha kalori 200- sawa na donati, aina ya maandazi.
Hata hivyo idadi kubwa ya watu hawajui madhara ya kula kiwango kikubwa cha kalori.
Waziri wa Afya Jane Ellison amesema "hatua kubwa" imefanyika kwa kuviwekea nembo vyakula, na kwa suala hilo serikali italiangalia.
Sekta ya vinywaji imesema imesema iko tayari kwa wazo hilo la kuweka nembo zenye kuonyesha kiasi cha kalori, lakini kuweka nembo zinazonyesha kiwango cha kilevi katika kinywaji ni muhimu zaidi.
Uingereza ni moja ya mataifa yenye watu wenye unene wa kupita kiasi duniani kwa kuwa na idadi ya karibu robo ya watu wazima kuwekwa katika kundi la wenye unene wa kupitiliza.
Vyakula tayari vinakuwa na taarifa za kiasi cha kalori kilichomo ndani yake, lakini pombe haimo katika sheria za Umoja wa Ulaya zinazotaka vyakula viwekewe nembo.
Mvinyo nao watakiwa kuonyesha kiwango cha kalori
Na Tume ya Ulaya inaangaliwa iwapo vinywaji viwekewe nembo yenye kuonyesha kiasi cha kalori kilichomo.
Utafiti uliofanywa na Chama cha Masuala ya Afya ya Jamii nchini Uingereza, umesema hatua hii itaungwa mkono na wanywaji nchini Uingereza.
Mkuu wa chama hicho cha RSPH, Shirley Cramer, ameiambia BBC: "Ni jambo la kushtusha kweli - asilimia 80% ya watu wazima hawana wazo la kujua kiasi cha kalori kilichomo katika kinywaji chochote na kama wanafikiri wana wazo hilo kwa ujumla wanakadiria kiasi cha chini mno."
"Itasaidia taifa kupunguza watu wenye unene wa kupitiliza na huenda kupunguza kupunguza unywaji wa pombe."

Kiasi cha kalori:

Glasi kubwa ya 250ml ya mvinyo wenye kileo cha asilimia 8% ni kalori 170 Kiasi hicho hicho cha glasi ya 250ml ya mvinyo wenye kileo cha asilimia 14% ni kalori 230 Painti moja yenye asilimia 4% ya bia ni zaidi ya kalori 180

Rais wa Burkina Faso ameng'olewa mamlakani

Kuna hofu kuwa rais Compaore anataka kuendelea kushikilia madaraka
Msemaji wa jeshi amewaambia waandishi wa habari mjini Ouagadougou kuwa bwana Compaore hayuko mamlakani tena.
Rais Compaore alikuwa ametangaza kuwa atajiuzulu baada ya kipindi cha serikali ya mpwito ya mwaka mmoja .
Lakini wanasiasa wa upinzani wakakataa kata kat kuendelea kwa utawala wake na wakamtaka ajiuzulu maramoja.
Rais Compaore alikuwa ameongoza kwa zaidi ya miaka 27 tayari.
Kumeripotiwa maandamano mapya nchini Burkina Faso ya kutaka kujiuzulu mara moja kwa rais wa nchi hiyo Blaise Compaore.
Viongozi wa upinzani wanakutana kwenye mkji mkuu Ouagadougou kukubaliana kwa pamoja hatua watakazochukua.
Siku ya Alhamisi waandanamaji walikarisishwa na jitihada za rais za kuongeza kipindi chake chake miaka 27 madarakani na wakateketeza bunge na kusaka kituo cha runinga cha serikali.
Rais Compaore ametangaza kuvunjwa kwa serikali na bunge
Bwana Compaore alitupilia mbali jitihada za kubadilisha katiba ambayo ingemruhusu kuwania tena muhula mwingine kama rais lakini akasema kuwa atabaki madarakani kwa mwaka moja zaidi .
<span >Viongozi wa Upinzani Nchini Burkina Faso wamewaomba waandamanaji kutolegeza kamba bali kuendelea na maandamano huku wakimtaka Rais Blaise Campaore ang'atuke mamlakani mara moja.
Licha ya Rais Compaore wa Burkina Faso kuhutubia taifa siku moja baada ya vurugu kubwa na kutangaza kuvunja serikali waandamanaji hawataki kusikia kwamba apewe muda wa mwaka mmoja ndipo aondoke madarakani.
<span >Jana jioni kiongozi wa Jeshi J<span >eneral Honore Traore alitangaza kuundwa kwa serikali ya mpwito itakayodumu kwa kipindi cha mwaka mmoja japo hakusema ninani atakayeiongoza.

Jen.Traore ajitangaza rais Burkina Faso

Jenerali Honore Traore mkuu wa jeshi la Burkina Faso aliyejitangaza rais mpya wa nchi hiyo
Mkuu wa Jeshi la Burkina Faso Jenerali Honore Traore sasa amejitangaza kuwa rais baada ya aliyekuwa rais wa Burkina Faso Blaise Compaore kutangaza kujiuzulu.
Jenerali Traore ameshinikizwa na waandamanaji ambao walikuwa wanamtaka kuchukua usukani baada ya kuondoka kwa Bwana Compaore.
Bwana Compaore amesema kuwa amekubali kuondoka madarakani ili kutii matakwa ya waandamanaji ambao hawamtaki kuendelea kuongoza taifa hilo hata baada ya kutawala kwa miaka 27.
Bwana Compaore sasa ametaka uchaguzi mpya wa urais ufanyike baada ya siku 90.
Awali msemaji wa jeshi alikuwa amewaambia waandamanaji kuwa bwana Compaore hayuko tena madarakani huko Ouagadougou.
Maelfu ya waandamanji walikuwa wamerejea mabarabarani kwa siku ya pili
Hata hivyo hakubaini ikiwa afisa huyo wa kijeshi alikuwa akizungumza kwa niaba ya jeshi lote.
Jeshi lilisema kuwa litafanya mkutano na waandishi habari.
Siku ya Alhamisi waandamanaji waliokuwa wamekasirishwa na jitihada za rais za kuongeza muda wa uongozi wake baada ya kutawala kwa miaka 27 waliteketeza jengo la bunge na kuvamia kituo cha televisheni ya taifa.
Bwana Compaore alitupilia mbali jitihada za kubadilisha katiba ambayo ingemruhusu kuwania tena muhula mwingine kama rais lakini akasema kuwa angebaki madarakani kwa mwaka moja zaidi.

Why always him: Exclusive pictures show inside of Mario Balotelli's burnt out bathroom after fireworks were let off inside £16million striker's Cheshire mansion


  • .MailOnline picture exclusive shows scale of damage indoor fireworks display caused to Mario's £3m rented mansion 
  • .Liverpool star said that a friend set off explosions in the bathroom, which is believed to have caused £400,000 damage 
  • .The next day he scored twice against rivals Manchester United revealed a t-shirt with the message: 'why always me?'
Pictures published by MailOnline for the first time today show how the indoor display started a fire that destroyed rooms in his £7,500-a-month house in Mottram St Andrew, Cheshire, causing a reported £400,000 of damage.
A friend of the millionaire footballer set off dozens of fireworks from 'multi-shot barrage cannons' in his first floor bathroom three years ago, starting a serious blaze.
Despite the fire he scored twice against rivals Manchester United on the day after the firework incident and Balotelli revealed a t-shirt with the cryptic message: 'why always me?' 

Carnage: This is Mario Balotelli's wrecked bathroom in his £3million mansion after a friend destroyed it with a pre-bonfire night fireworks display 

Chaos: This picture shows where the mansion's bath was and tiles and plaster appear to have been blown off the wall and ceiling 
Balotelli asked: Why always me after the fire
Party: These are the 'barrage cannons' of fireworks set off in the bathroom, which wrecked the first floor and started a blaze on the eve a huge game again Manchester United. Balotelli scored twice and used this t-shirt to ask: Why always me?
Bathroom towels were set on fire and the flames spread but Balotelli has insisted that he did not cause the blaze and that the offending fireworks were let off by his friends.
New photographs appear to show how tiles and plaster were blown off the walls and ceilings, the walls were scorched and covered in soot and how the landlord had to rip out fittings and start again. 
Balotelli's four-bedroom house, where he no longer lives, suffered severe smoke damage and the bathroom was gutted in the fire, which needed ten firefighters with breathing apparatus to put it out.
The indoor display happened in the early hours on the eve of Manchester City's top-of-the-table derby clash at Old Trafford in October 2011.
The controversial Italian and his friends escaped unhurt after fleeing the fire at 1am,  

Bedroom: Smoke and soot damaged the walls, ceilings and fittings in the mansion in Cheshire's stockbroker belt  

Description: Balotelli said that he had put the fireworks in a bin in the bathroom, right and left, but left the room and one of his friends lit them 

Danger: At the time it was reported that the Liverpool striker had been asked to pay £400,000 to the landlord for the damage caused 
The scorched and dirty walls and carpets of the mansion
Trashed: These picture show the fire damage caused to the bathroom's shower cubicle and the carpets and walls of neighbouring rooms
Liverpool's eccentric striker had a rocket from his landlord, who wanted Balotelli, 24, demanded the Italian international pay for the estimated £400,000 repairs himself rather than go through insurance.
Describing what happened in an interview with Noel Gallagher on the BBC he said: 'I was bored no, so I was with my friends and one of them was limping so I got one bin you know the bin? For put fireworks inside.
'But nothing gonna happen right, so I left the room and I left the fireworks but I didn't I walk out and then my friend go in the room and they just start screaming blah blah blah and the fireworks was going off and they put the fireworks on the bed, not on the bed sorry, on the toilet.
'But just the curtain caught on fire, that's it, nothing else. Just the toilet was lost'. 
Balotelli has been the subject of controversy since being in English football, playing for Manchester City before being sold back to AC Milan. He returned to the Premier League this summer in a £16million move to Liverpool. 
Having scored at Old Trafford, Balotelli unveiled a T-shirt which read 'Why Always Me?' in response to the scrutiny he finds himself under due to his tendency to prompt negative headlines.
Aftermath: The controversial Italian and his friends escaped unhurt after fleeing the fire at 1am three years ago
Aftermath: The controversial Italian and his friends escaped unhurt after fleeing the fire at 1am three years ago
Response: Despite the unfortunate incident at home Mario was chosen to front a firework safety campaign days later
Response: Despite the unfortunate incident at home Mario was chosen to front a firework safety campaign days later


Hobbies: Balotelli also had scooters and a motorbike in the house, as well as a remote control car on the shelf
He was disciplined by the club for throwing darts at a youth team player in 2010, while he was also pictured trading punches on the training ground with former team-mate Jerome Boateng. He has paid a total of £300,000 in club fines.
In April 2011, it was reported Balotelli had spent £10,000 in parking fines and had his sports car impounded 27 times.
Liaison officials at the club were forced to reclaim the Maserati time and time again as the player was given an average of three parking tickets a day since joining the Premier League club.
He once crashed his sports car soon after arriving and it was reported that police found £5,000 in cash in his back pocket.
The striker was reprimanded for throwing darts at the training ground.