Na Mwandishi
wetu_MAELEZO-Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Profesa Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa kituo cha michezo katika eneo la Kidongo
Chekundi jijini Dar es Salaam.
Kituo cha michezo kinajengwa kwa
ufadhili wa Klabu ya Sunderland kwa kushirikiana na Symbion Power na Serikali
ya Tanzania.
Shehere hizo zinatarajiwa kesho
asubuhi (Jumamosi tarehe 1 Novemba 2014) kuanzia majira ya saa mbili asubuhi.
Kwa mijbu wa taarifa iliyotolewa
leo jijini Dar es salaam na Mwakilishi wa Symbion nchini Julie Foster , sherehe
hizo pia zitahudhuriwa na Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt.
Fenella E. Mukangara, Afisa
Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Sunderland ya Nchini Uingereza Bi. Margaret Byrne na Afisa Mtendaji Mkuu wa Symbion Power Bw. Paul
Hinks
Taarifa hiyo imeongeza kuwa
pamoja na uzinduzi wa ujenzi huo Rais Kikwete atapanda mti kwenye eneo hilo,
akisaidiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Sunderland AFC Bi. Byrne, Mkurugenzi wa Biasharawa
klabu hiyo Gary Hutchinson, na Afisa Mtendaji Mkuu wa Symbion Power Bw. Hinks.
Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza ya
Barclays, Sunderland AFC inatoa usaidizi wa kiufundi na utendaji katika
uendelezaji wa mradi wa mpira wa miguu, ambao ni wa kwanza na wa aina yake
nchini humu, utakaohakikisha maelfu ya
vijana wananufaika kutokana na mtazamo wa pamoja wa kuchanganya mpira wa miguu,
elimu na ushiriki wa jamii, ili kupata ujuzi na utaalam wa Sunderland AFC.
No comments:
Post a Comment