Meneja wa Miradi, Usambazaji na Usafirishaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Emmanuel Manderabona, akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani), moja ya transfoma, iliyopo katika eneo la mradi wa Mbagala, yenye uwezo wa MVA 50. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba. (PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO)
Baadhi
ya mafundi wakiedelea na kazi ya kusuka Transfoma iliyopo katika eneo la Mradi
Mbagala lenye MVA (MEGAVOLT-AMPERE) 50.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba
akiwaeleza waandishi wa Mikakati inayowekwa na shirika hilo ikiwemo kutekeleza
miradi mbalimbali ya kuzalisha, kusafirisha na kusambaza Umeme ili kuhakikisha
wanakabiliana na Tatizo la Umeme Nchini,wakati wa Ziara kwenye Mradi wa “Tanzania Energy Development and Access
Program (TEDAP)” unaotekelezwa
katika maeneo ya Mbagala, Gongo la Mboto na Kinyerezi, Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiwaeleza waandishi wa habari
kufurahishwa kwake na ziara hii iliyoratibiwa Wizara ya Habari, Vijana ,
Utamaduni na Michezo kwa kushirikiana na Shirika la umeme Tanzania (TANESCO)
yenye lengo la kuona nini Shirika hilo linatekeleza katika jitihada za
kukabiliana na Tatizo la Umeme Nchini.Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akimweleza jambo Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba (kushoto) wakati wa ziara kwenye Miradi ya umeme Katika
Eneo la Mbagala, Gongo la Mboto na Kinyerezi Jijini Dar es Salaam.
Afisa
Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bi. Neema Mbuja akiwaeleza
jambo wahandisi Emmanuel Manderabona(Kushoto kwake) na Saimon Jilima, wakati wa
ziara kwenye Miradi ya umeme Katika Eneo la Mbagala, Gongo la Mboto na
Kinyerezi Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Miradi, Usambazaji na Usafirishaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) Emmanuel Manderabona akiwaonesha waandishi wa habari mtambo wa
kuongoza umeme uliopo katika eneo la Gongo la Mboto uliowekwa mfumo wa Sakiti
Mzunguko (Ring Circuit) kwenda Mbagala, Sakiti Mzunguko ni Mzunguko mkubwa utakaotoa
fursa ya upatikanaji wa umeme kwa muda wote kwani umeme ukikosekana eneo moja
ni rahisi kuunganisha kwa kupitia upande wa pili na umeme ukaendelea
kupatikana.
Mitambo Miwili iliyofungwa katika kituo cha Kinyerezi One, yenye uwezo wa kuzalisha Megawatt 150 za umeme utakaogawanywa katika sehemu mbili kuingia katika gridi ya Taifa, ikiwa ni kujenga msongo wa kilovolt 220 kwenda Kimara na kujenga laini ya msongo wa kilovolt 132 kwenda Gongo la Mboto, Kituo hiki kitagharimu Dola za Kimarekani Milioni 183. (Picha zote na Hassan Silayo-MAELEZO)
No comments:
Post a Comment