*Dk. Shen: Tutaendelea kuhakikisha malengo ya Elimu katika mipango yote ya maendeleo yanatekelezwa
Baadhi ya wanafunzi wa Skuli mbalimbali za Sekondari wakiwa katika jukwaa wakati wa sherehe za Miaka 50 ya Elimu bila malipo zilizofanyika kitaifa katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja leo.Baadhi ya Viongozi waliohudhuria katika sherehe za miaka 50 ya Elimu bila Malipo zilizofanyika katika uwanja wa Amaan Studium na mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Baadhi ya walimu wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipokuwa akizungumza na Walimu, Wazee,Wanafunzi katika sherehe za kilele cha miaka 50 ya Elimu bila Malipo zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Zanzibar.
Wanafunzi wenye ulemavu tofauti wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa maandano wakati wa sherehe za miaka 50 ya Elimu bila Malipo zilizofanyika katika uwanja wa amaan Studium
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wanafunzi waliopita mbele ya jukwaa la viongozi katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Zanzibar wakati wa sherehe za kilele cha miaka 50 ya Elimu bila Malipo zilizofanyika leo.
Walimu na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa SUZA wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati wa maandamo ya kusherehekea kilele cha miaka 50 ya Elimu bila malipo ilizofanyika katika uwanja wa amaan Studium
Wanafunzi wa Chuo cha Ufundi JKU wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akipokea maandamano ya wanafunzi wa skuli mbali mbali za Unguja na Pemba katika sherehe za miaka 50 ya Elimu bila malipo zilizofanyika kitaifa katika uwanja wa Amaan Studium leo.
Wanafunzi wa Skuli ya wanawake ya Al- Ihsaan ya Magogoni Jitmai wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akipokea maandamano ya wanafunzi wa skuli mbali mbali za Unguja na Pemba katika sherehe za miaka 50 ya Elimu bila malipo zilizofanyika kitaifa katika uwanja wa Amaan Studium leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Walimu na Wanafunzi katika Sherehe za Miaka 50 ya Elimu bila malipo zilizofanyika kitaifa katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Walimu na Wanafunzi katika Sherehe za Miaka 50 ya Elimu bila malipo zilizofanyika kitaifa katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi kombe Msaidizi Afisa Elimu Mkoa wa Kaskazini Unguja Maulid Nafasi Juma wakati wa Sherehe za Miaka 50 ya Elimu bila malipo zilizofanyika kitaifa katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja leo.
Na Said Ameir, Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewahakikishia wananchi wa Zanzibar kuwa Serikali imejidhatiti kuhakikisha kuwa malengo yote katika mipango ya maendeleo ya nchi yanayohusu uimarishaji wa elimu yanafikiwa na kutoa matokeo yanayotarajiwa.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewahakikishia wananchi wa Zanzibar kuwa Serikali imejidhatiti kuhakikisha kuwa malengo yote katika mipango ya maendeleo ya nchi yanayohusu uimarishaji wa elimu yanafikiwa na kutoa matokeo yanayotarajiwa.
Akihutubia maelfu
ya wananchi katika kilele cha Maadhimisho ya Miaka 50 ya Elimu bila Malipo yaliyofanyika
kwenye uwanja wa Amaan mjini Unguja leo, Dk. Shein amesema Serikali inatambua
kuwa mafanikio ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya nchi yanategemea
kuimarika kwa kiwango cha elimu hivyo ndio maana suala la uimarishaji wa elimu
limepewa kipaumbele katika mipango mbalimbali ya maendeleo.
Aliitaja
mipango hiyo kuwa ni pamoja na Dira ya Maendeleo 2020, Mpango wa Kukuza
Uchumi na Kupunguza Umasikini (MKUZA II),Mpango wa Maendeleo ya Elimu,
Malengo ya Milenia ya Elimu na Ilani ya Uchaguzi ya CCM mwaka 2010.
Katika kufanya
hivyo, aliwaambia wananchi kuwa Serikali itaendelea kuongeza nafasi za masomo
katika viwango vyote kuanzia skuli za maandalizi hadi chuo kikuu ili kutoa
fursa kwa kila mtoto kupata elimu katika ngazi zote.
Sambamba na kuongeza
fursa za masomo, kwa upande mwingine alisema Serikali inafanya jitihada kubwa
kuhakikisha ubora wa elimu inayotolewa katika ngazi zote unazidi kuongezeka kwa
kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha mazingira ya utoaji elimu nchini.
Alizitaja hatua
hizo kuwa ni pamoja na kuzipatia skuli vifaa na nyezo za kisasa za kufundishia
ikiwemo vitabu, vifaa vya maabara, kompyuta na walimu bora ili kuwawezesha wanafunzi
kufaulu masomo yao vyema.
Dk. Shein alitoa
mfano wa hatua mzuri iliyofikiwa katika kuwapatia wanafunzi vitabu katika skuli
za sekondari ambapo alieleza kuwa kushirikiana na Benki ya Dunia na Serikali ya
Marekani hivi sasa kila mwanafunzi katika ngazi hiyo ana vitabu vya masomo
anavyovidhibiti mwenyewe na kwenda navyo nyumbani.
Katika hotuba yake
hiyo, Dk. shein alitoa wito kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuendeleza
juhudi za ufundishaji wa taaluma ya tekinolojia ya habari na mawasiliano katika
skuli za Unguja na Pemba ili Zanzibar iweze kwenda sambamba na maendeleo na
mabadiliko ya karne 21 ambayo yanazingatia matumizi ya tekinolojia hiyo.
Hata hivyo ameitaka
wizara hiyo kuwa mstari wa mbele katika kudhibiti matumizi kwa kutunga kanuni
zinazokataza matumizi mabaya ya mitandao na simu za mikononi kwa wanafunzi
maskulini.
Kuhusu maslahi ya
walimu, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliwahakikishia
walimu kuwa Serikali itaendelea kuimarisha mazingira ya kufanyia kazi kwa
kuwapatia mafunzo zaidi pamoja na kuwaongezea mishahara kadri uchumi unavyokua
na hali inavyoruhusu.
Dk. Shein
alizungumzia pia suala la ukosefu wa ajira kwa wahitimu wengi wanaomaliza vyuo
mbali mbali huku akitambua changamoto inayowakabili wengi wa wahitimu hao ya
kukosa maarifa ya kutosha kujiajiri hivyo kutegemea ajira.
Kwa upande wake
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Awali Bibi Zahra Ali Hamad alieleza
mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika sekta ya elimu na kuongeza kuwa ongezeko
kubwa la bajeti ya elimu mwaka hadi mwaka ni hatua inayodhihirisha umakini wa
Serikali katika kuimarisha elimu nchini.
Tarehe kama leo 1964,
miezi tisa baada ya Mapinduzi ya Zanzibar, Rais wa kwanza wa Zanzibar marehemu
Sheikh Abeid Amani Karume alitangaza elimu bila malipo kwa kila mwananchi na
kuondosha kabisa ubaguzi katika mfumo wa elimu Zanzibar.
Mapema Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiri wa Baraza la Mapinduzi alipokea maandamano ya wanafunzi kutoka
skuli mbalimbali za Unguja na Pemba na baadae kufuatiwa na burudani za vikundi
vya sanaa na michezo.
No comments:
Post a Comment