Ofisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu (katikati), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo kuhusu miradi ya Barabara iliyotekelezwa na manispaa kwa ajili ya kupunguza msongamano wa magari. Kushoto ni Mhandisi wa Manispaa hiyo, James Batinagwa na kulia ni Ofisa Habari, Idara ya Habari, Maelezo, Frank Mvungi.
Ofisa Habari, Idara ya Habari, Maelezo, Frank Mvungi, akizungumza na waandishi wa habari, wakati viongozi wa Manispaa ya Ilala, walipokuwa wakizungumza nao, Dar es Salaam leo. Katikati ni Ofisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu na kulia ni Mhandisi wa Manispaa hiyo, James Batinagwa.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa katika mkuano huo.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo leo.
Ofisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu (katikati), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo.
Ofisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu (katikati), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati wa viongozi wa Manispaa hoyo, walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa kweye mkutano huo, wakifuatilia masuala mbalimbali kwenye manispaa hiyo, Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa kweye mkutano huo, wakifuatilia masuala mbalimbali kwenye manispaa hiyo, Dar es Salaam leo. Kulia ni Ofisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu.
Ofisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu, akizungumza kwenye mkutani.
Ofisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa kwenye mkutano huo, Dar es Salaam leo.
HALMASHAURI YA MANISPAA YA
ILALA
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kupitia Idara ya Ujenzi inahudumia
barabara zenye urefu wa kilomita 536.9 ambazo kati ya hizo kilomita 144.2 ni za
lami, kilomita 64.7 ni za Changarawe na kilomita 328 ni za udongo. Huduma hizi ni pamoja na kujenga, kukarabati
na kusimamia sheria za matumizi ya barabara katika eneo la Manispaa ya Ilala.
MIRADI ILIYOTEKELEZWA HADI SASA KWA AJILI YA KUPUNGUZA
NSONGAMANO
Ujenzi wa Barabara ya Mazengo hadi Kibasila kwa kiwango cha Lami Km.1.2
Ujenzi wa Barabara ya Lindi kwa kiwango cha Lami Km. 0.7
Ujenzi wa barabara ya Vingunguti
Baracuda- urefu wa 1.3 km unaendelea na tayari mita 880 ziko hatua
kuanza kuweka lami nyepesi na lami ngumu.
UCHONGAJI WA BARABARA ZA UDONGO
Halmashauri imeweza kutekeleza kazi za uchongaji wa barabara za udongo
na changarawe kwa kutumia greda lake moja.
Barabara zilizochongwa ni za maeneo ya kata za Ukonga, Pugu, Majohe,
Kivule, Msongola, Chanika, Kitunda, Kinyerezi, Tabata, Kimanga, Gongolamboto,
Kipawa, Kiwalani, Vingunguti, Upanga Mashariki, upanga Magharibi, Gerezani
Ilala, Jangwani, Mchikichini na Buguruni. Barabara hizi zimekuwa zikiharibika
wakati wa kipindi cha mvua zinapokuwa nyingi mathalani mvua zilizonyesha katika
Mkoa wa Dares Salaam na kuleta maafa. Barabara nyingi ziliharibika kiasi cha
kutopitika kabisa hali iliyoathiri huduma mbalimbali.
Kwa kuliona hilo na kuhakikisha kuwa Barabara hizi zinapitika wakati
wote Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imenunua Magreda mawili (2) kwa gharama
ya Tshs 1.2 billioni. Pamoja na jitihada hizo yapo maeneo mawili ambayo kwa sasa
ni kero
ENEO LA HYDARI PLAZA
Eneo hili hujaa maji wakati wa Mvua kutokana na kuwepo kwa Chemba za
Maji taka zinazotiririsha maji barabarani na kusababisha mashimo ambayo
yamekuwa adha kwa watumiaji wa barabara hiyo. Halmashauri imekuwa ikiziba
viraka vya lami bila mafaikio. DAWASCO ambao ndiyo wamiliki wa chemba hizo
wametakiwa kuzikarabati chemba zao. Halmashauri
inaendelea na maandalizi ya kuweka zege badala ya lami ili eneo hilo liweze
kupitika kwa urahisi. Kazi hii
itafanyika mapema katika mwaka huu wa fedha 2014/2015.
ENEO LA SHULE YA UHURU WASICHANA HADI UHURU
MCHANGANYIKO – BARABARA YA LINDI
Eneo hili lilifanyiwa ukarabati wa mfereji wa maji ya mvua ili
kuyaingiza katika kalavati kuu lilopo katikati ya barabara ya Mismbazi, kisha
lami iliwekwa. Lakini kufuatia eneo hilo
kutumiwa na Daladala za Temeke/Tandika – Kariakoo bila udhibiti wa kutosha wameharibu
mferefi huo na kusababisha maji kutuama na kuharibu tabaka lote la lami, Halmashauri ina kusudia kuujenga upya mfumo
wa maji ya mvua na kuweka lami kipande hicho katika mwaka wa fedha 2014/2015.
MASHIMO YA BARABARANI
Uchakavu wa barabara za lami hasa maeneo ya katikati ya Jiji (Kata na Gerezani,
Kivukoni, Kisutu, Mchafukoge, Jangwani, Kariakoo, Upanga mashariki na
magharibi). Hali hii inatokana na barabara nyingi katika maeneo haya kuchoka
(kuzeeka) kwani nyingi zilijengwa katika miaka ya 1990. Uchakavu huu unachangia
kuwepo kwa mashimo mengi kwakuwa zinaharibika kwa wakati mmoja.
Jambo lingine linalochangia uharibifu wa barabara na kuwa na mashimo ni
ukataji ovyo wa barabara kwa lengo la kuweka na kukarabati miundombinu ya maji
safi na taka na mikonga ya mawasiliano ya simu. Wakandarasi ambao hurusiwa
kufanya kazi hiyo huchukua muda mrefu kurejesha barabara katika hali ya awali.
Hali inasababisha maji ya mvua kutuama na kuharibu tabaka la barabara. Halmashauri
imekuwa ikiyaziba mashimo hayo kulingana na hali ya upatijanaji wa fedha, Hata
hivyo bado hali haijawa bora kwani Barabara hizi zinahitaji matengenezo makubwa
ya kuwekwa Lami upya.
CHANGAMOTO
·
Uhaba wa fedha za kukidhi mahitaji ya matengenezo
mapya na ukarabati wa barabara, madaraja makalavati na mifereji ya maji ya mvua
ukilinganisha na ukubwa wa mtandao wa barabara.
·
Ukataji holela wa barabara kwa malengo ya kuweka
mifumo ya maji safi, maji taka, mawasiliano (fibre cables), n.k kinyume cha
utaratibu ambapo Halmashauri hutoa vibali na kusimamia urejeshaji wa
miundombinu iliyoharibiwa.
·
Wizi wa mifuniko ya chemba za maji ya mvua kwa ajili
ya biashara ya chuma chakavu.
·
Utupaji ovyo wa taka na michanga barabarani, hali hii
inasababisha kuziba kwa mifereji ya maji ya mvua na kusababisha uharibu wa
barabara kutokana na mafuriko, madibwi makubwa ya maji. Hii ni kero kwa watumiaji wa barabara.
·
Wananchi kuunganisha mfumo wa maji taka ya majumbani
kwenda mifereji ya maji ya Mvua. Hususan
katika Kata za Gerezani, Kariakoo, Jangwani, Kisutu na Mchafukoge ambapo baadhi
yao wamekamatwa na kutozwa faini na kisha kuziba mifumo hiyo. Kitendo hiki kinasababisha kuwepo kwa harufu
mbaya katika maeneo mbalimbali kwa watumiaji wa Barabara.
Mikakakati
·
Halmashauri inaendele a kuweka mifuniko ya mifereji ya
maji ya mvua. Hadi sasa jumla ya mifuniko 410, ambapo 250 imewekwa kwenye
chemba zilizo kuwa wazi na 160 ipo kwa ajii ya dharura
·
Kujenga mifereji mipya ya maji ya mvua katika sehemu
korofi.
·
Kuunda kitengo kitakachodhibiti uzito wa magari kwa
kuweka mizani zinazohamishika katika maingilio yote ya barabara kuu za kuingia
katikati ya Halmashauri kwa masaa 24.
Imeandaliwa na;
Tabu F.Shaibu- Afisa Uhusiano
No comments:
Post a Comment