TANGAZO


Wednesday, September 3, 2014

Wozniacki afika nusu fainali US Open

Wozniacki mefuzu kwa mara ya kwanza katika miaka mitatu iliyopita

Mcheza Tennis wa Denmark,Caroline Wozniacki ameingia kwenye nusu fainali ya mashindano ya tennis kwa kumshinda mchezaji bora wa 13 duniani Sara Errani wa Italia kwa pointi, 6-0 6-1 .
Wozniacki, anayeorodheshwa wa kumi miongoni mwa wachezaji bora zaidi duniani, alishinda mechi yake katika dakika 65 na kujinyuakulia nafasi katika nusu fainali.
Bingwa huyo wa zamani wa dunia sasa atacheza na Peng Shuai, wa China ambaye alifika nusu fainali yake ya kwanza ya mashindano hayo kwa kumcharaza

Belinda Bencic wa Usiwizi kwa seti mbili za pointi 6-2 6-1.
Peng, mwenye umri wa miaka 28, alinukuliwa akisema amefurahi sana kwa kufika nusu fainali.
Katika mechi zengine za nusu fainali, ambazo zitechezwa Jumatano, Serena Williams atamenyana na Flavia Pennetta huku Victoria Azarenka akichuana na Ekaterina Makarova.
Wozniacki, ambaye ameingia katika nusu fainali kwa mara ya kwanza katika miaka mitatu, alisema kuwa hii ni hatua kubwa sana kwake.
"msimu huu umekuwa na misukosuko sana kwangu na kuweza kufika hapa najisikia vizuri sana.

No comments:

Post a Comment