TANGAZO


Wednesday, September 3, 2014

Ufisadi ni jinamizi linaloua wengi

Pesa zinazopora zinaweza kuwasaidia mamilioni ya watu katika mataifa yanayostawi

Inakisiwa dola Trilloni 1 huporwa kutoka kwa nchi maskini kila mwaka huku maisha ya mamilioni ya watu katika nchi hizo yakihatarishwa.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la kupambana na umaskini la 'Organisation one'.
Matukio ya ufisadi ni pamoja na utumiaji wa makampuni ghushi na utengezaji wa pesa kwa njia haramu.Shirika hilo linasema kwamba faida zilizofikiwa katika kupambana na umaskini katika miongo miwili iliyopita, zinakabiliwa na tisho kubwa kwa sababu ya viwango vya juu vya ufisadi na uhalifu.
Ripoti hiyo inalaumu ufisadi kwa vifo vya watu milloni 3.6 kila mwaka.
Shirika hilo kadhalika linasema kwamba laiti hatua zingechukuliwa kukomesha vyanzo vya ufisadi kukita mizizi na pia kama mapato yaliyopatikana yangetumiwa kwa miradi ya afya - vifo vingi vingeweza kuzuiwa kwa nchi zenye mapato ya chini.
Vile vile shirika hilo linanukuu kuwa ufisadi unazidi kukithiri na kushinda majanga na maradhi yanayolemea mataifa maskini duniani na hata kutaja matokeo ya ripoti yake kama kashfa ya mabilioni ya dola.
Ripoti hiyo inanukuu: ''Ufisadi huzuia uwekezaji wa sekta binafsi,kupunguza kasi ya kukuwa kwa uchumi,huongeza gharama za kufanya biashara na inaweza kusababisha migogoro ya kisiasa.
Lakini katika mataifa yanayostawi, ufisadi ni jinamizi kubwa. Wakati serikali inapokosa kupata rasilimali za kutosha kuwekeza katika miradi yake ya afya, chakula, usalama,na miundo mbinu, kutokana na ufisadi, gharama ya maisha hupanda na watoto ndio wenye kuathirika zaidi.''
Shirika la One Organisation linasema kuwa iwapo ufisadi unaweza kutokomezwa katika mataifa ya kusini mwa jangwa la Sahara:
-Watoto wengine zaidi ya millioni kumi wataweza kupata elimu kila mwaka.
-Pesa za ziada zitapatikana ili kuwalipa walimu 500,000 wa shule za msingi
-Watu zaidi ya millioni 11 walioathirika na ugonjwa wa ukimwi wataweza kupata dawa za kupunguza makali ya Ukimwi.

No comments:

Post a Comment