Jengo
la gorofa 8 lenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.9 lililojengwa na
wakala wa Majengo Tanazania (TBA) Katika neneo la Ada Estate Kinondoni Jijini
Dar es Salaam ambalo litapangishwa kwa watumishi wa umma mara litakapokamilika
mwishoni mwa mwaka huu ikiwa ni moja ya hatua za Serikali kutatua tatizo la
makazi kwa watumishi wa umma.
Mafundi
wakiendelea na ujenzi katika mradi wa nyumba zaidi ya 150 zinazojengwa na TBA
ambapo nyumba hizo zitauzwa kwa watumishi wa umma ikiwa ni moja ya mikakati ya
Serikali katika kuondoa tatizo la makazi kwa watumishi hao.
Mhandisi
Edwin Nnunduma toka wakala wa amajengo Tanzania (TBA)akiwaeleza
waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba mbili zinajengwa katika kila mkoa kwa ajili ya
makazi ya majaji wakati wa ziara ya waandishi hao iliyolenga kujionea hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo.
Moja
ya jengo la kisasa lenye gorofa 4lililopo Mbezi beach Dar es Salaam
litakalopangishwa kwa watumishi wa Umma,jengo hilo liko katika hatua za mwisho
kabla kuanza kupangishwa ili kupunguza
tatizo la makazi kwa watumishi hao.
Mhandisi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Bw. Edwin Nnunduma akiwaongoza waandishi wa habari kutembelea
mradi wa ujenzi wa nyumba zaidi ya 150 zinazjengwa katika eneo la Mabwe Pande
Jijini Dar es salaam ambapo nyumba hizo zitauzwa kwa watumishi wa umma.
Mafundi
wakiendelea na ujenzi katika mradi wa nyumba zaidi ya 150 zinazojengwa na TBA
ambapo nyumba hizo zitauzwa kwa watumishi wa umma ikiwa ni moja ya mikakati ya
Serikali katika kuondoa tatizo la makazi kwa watumishi hao.
Mhandisi Edwin Nnunduma toka wakala wa amajengo Tanzania (TBA) akitoa
ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu lengo la mradi wa nyumba zaidi ya 150
katika eneo la Mabwepande ambapo nyumba hizo zitauzwa kwa watumishi wa umma
ikiwa ni sehemu ya mpango wa Serikali kupitia wakala huo kujenga nyumba 10,000.
Sehemu
ya nyumba 150 zitakazouzwa kwa watumishi wa umma ambapo mradi wa ujenzi wake unatekelezwa na
TBA katika eneo la mabwe pande jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya
waandishi wa habari wakiwa mbele ya moja
ya nyumba za Majaji zinazojengwa na TBA wakati wa ziara yao katika eneo
la masaki jijini Dar es salaam ili kujionea hatua iliyofikiwa katika
miradi inayotekelezwa na wakala huo, ambapo wakalo huo unajenga nyumba
mbili kila
Mkoa ili kukabliana na tatizo la makazi kwa Majaji hapa nchini. (Picha
zote na Frank Mvungi-Maelezo)
No comments:
Post a Comment