TANGAZO


Friday, September 26, 2014

Timu ya Michezo ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo yapaswa kuwa mfano katika mashindano ya SHIMIWI

Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasirimali Watu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Titus Mkapa akimkaribisha Mwenyekiti wa timu ya Wizara HUM Sports Club (hayupo pichani) ili atoa salama za wachezaji kwa mgeni rasmi wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wachezaji wa timu hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (HUM Sports Club) Dkt. Margareth Mtaki akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kuwaaga wachezaji wa timu hiyo inayotarajiwa kuondoka kesho kuelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya mshindano ya SHIMIWI leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Sihaba Nkinga na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza jambo wakati wa hafla ya kuwaaga wachezaji wa timu hiyo inayotarajiwa kuondoka kesho kuelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya mshindano ya SHIMIWI leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Sihaba Nkinga.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akimkabidhi zawadi Mwanamichezo aliyeiletea Wizara ushindi katika mashindano ya SHIMIWI na Meimosi mwaka jana Bibi. Niuka Chande. Mchezaji huyo aliibuka mshindi katika michezo ya Draft na kurusha Tufe na kuiletea Wizara vikombe viwili. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel na Mwenyekiti wa Timu ya Wizara  Dkt. Margareth Mtaki.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akipokea vifaa vya michezo kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwaaga wachezaji wa timu ya Wizara hiyo wanatarajia kwenda mjini Morogoro kesho kwa ajili ya mashindano ya SHIMIWI yatakayoanza kuanzia tarehe 27 septemba hadi Oktoba 11.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akiwa amenyanyua juu  Kikombe  cha ushindi wa kwanza kwa mchezo wa Draft katika mashindano ya SHIMIWI mwaka jana ambacho kilinyakuliwa na mchezaji watimu ya Wizara ya Habari Bibi. Niuka Chande (mwenye taki suti nyeusi)kushoto Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel akifurahia.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya HUM Sports Club wakitoa salaam za timu yao kwa mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo hayupo pichani leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwaaga wachezaji wa timu hiyo wanakwenda mjini Morogoro kushiriki mashindano ya SHIMIWI yanayotarajiw kuanza tarehe 27 mwezi huu na kumalizika tarehe 11 Oktoba.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wachezaji wa timu ya Wizara itakayoshiriki mashindano ya SHIMIWI mwaka huu.Waliokaa kutoa kushoto ni Kaimu mkurugenzi wa TBC Joyceline Lugora, Mwakilishi wa Kampuni ya Water.Com(T) Ltd Juma Rajab Mboge, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel na Mwenyekiti wa Timu ya HUM Sports Club Dkt. Margareth Mtaki. (Picha zote na Frank Shija, WHVUM)


Na Anitha  Jonas - Maelezo
Timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo waaswa kuwa mfano katika mashindano ya SHIMIWI ikizingatiwa kuwa ipo chini ya Wizara inayo simamia michezo nchini.
Wito huo umetolewa leo jiji Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni  na Michezo, Bibi  Sihaba Nkinga wakati Timu hiyo ikiagwa rasmi kwa ajili ya kuelekea Mkoani Morogoro kwa kushiriki mashindano ya SHIMIWI 2014 yanayotarajiwa kuanza tarehe 27 Septemba hadi  tarehe 11 Oktoba.
Bibi Sihaba pia amewataka wanamichezo hao kuwa  na nidhamu katika michezo, kuzingatia sheria na kanuni zinazoongoza michezo watakayoshiriki  na kujituma kwa lengo la kuleta ushindi.

“Kumbukeni  kuwa ninyi ni  Watumishi wa Umma hivyo mnapaswa kuzingatia  maadili ya Utumishi wa Umma katika kutelekeza dhamira ya mashindano hayo”.Amesema Bibi Nkinga.


Kwa upande mwingine Bibi Sihaba amewashukuru wadhamini mbalimbali wakiwemo Platinum Credit Ltd, Starmedia (Startimes)TFF,WaterCom (T) Ltd na Mohamed Enterprise  kwa kushirikiana na Wizara kuinua michezo kwa kuchangia vifaa mbalimbali vya michezo ili kufanikisha mashindano hayo.

Naye Mwenyekiti wa Timu Dkt. Margret Mtaki ameushukuru  uongozi wa Wizara kwa kuwapa ushirikiano mzuri katika kufanikisha maandalizi ya Timu kwa  kuwapatia vifaa vya kutosha katika michezo yote.
Pia Mwenyekiti  ameahidi  kuwa Timu itazingatia  nidhamu ya hali ya juu na kujituma ili kuelete ushindi wa kishindo kwa Wizara.
Aidha, Mshindi wa Mchezo wa Drafti na Kurusha Tufe katika Mashindano ya SHIMIWI 2013 na Mashindano  ya Mei Mosi 2014  Bi. Niuka  Chande amekabidhiwa  zawadi ya sh. 300,000 na cheti cha kutambua mchango wake katika michezo hiyo na  kuiletea Wizara ushindi.
Timu ya Wizara mwaka huu inajumuisha jumla wachezaji 55 amabao watashiriki michezo mbalimbali ikiwemo  Mpira wa Miguu,Riadha,Mpira wa Pete, Drafti, Karata, Bao na Kuvuta Kamba.


No comments:

Post a Comment