TANGAZO


Wednesday, September 24, 2014

Uwasilishwaji wa Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa kwenye Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma leo

*Bunge Maalum lapendekeza Ibara 274 badala ya  271 za iliyokuwa Tume ya Katiba
*Ibara 186 za Tume zaboreshwa
*Ibara  41 ni mpya
*Ibara 47 za Tume zabaki kama zilivyokuwa
*Ibara 28 za Tume zafutwa

Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi, Mhe. Andrew Chenge (kushoto) akiwasili bungeni kwa ajili ya kuwasilisha Rasimu ya Katiba inayopendekezwa, leo 24 Septemba, 2014. Kulia ni mjumbe wa bunge hilo, Dkt. Tuli Jackson. (Picha zote na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma)



Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi, Mhe. Andrew Chenge (kushoto) akiwasili bungeni kwa ajili ya kuwasilisha Rasimu ya Katiba inayopendekezwa, leo 24 Septemba, 2014. Kulia ni mjumbe wa bunge hilo, Dkt. Tuli Jackson.

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akiongoza bunge hilo, leo 24 Septemba, 2014, mjini Dodoma.


Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akiongoza bunge hilo, leo 24 Septemba, 2014, mjini Dodoma.


Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishiwa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Andrew Chenge akiwasilisha Rasimu iliyopendekezwa ndani ya bunge hilo, leo 24 Septemba, 2014 mjini Dodoma.


Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishiwa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Andrew Chenge akiwasilisha Rasimu iliyopendekezwa ndani ya bunge hilo, leo 24 Septemba, 2014 mjini Dodoma.


Na  Mwandishi wa MAELEZO-Dodoma
Bunge Maalum la Katiba limependekeza jumla ya Ibara 274 katika Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayopendekezwa.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Mwenyekiti wa  Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalum Mhe. Andrew John Chenge wakati akiwasilisha Bungeni Rasimu ya Katiba inayopendekezwa katika Kikao cha Arobaini na mbili.
Amesema kuwa wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba inawasilisha Bungeni Rasimu Katiba inayopendekezwa iliwasilisha  Ibara 271.
Mhe. Chenge amesema kuwa baada ya kupitia Rasimu Katiba ya Tume walifanikiwa kupata Ibara 274 ambazo ndio wanapendekeza ziwemo katika Katiba mpya ijayo.
Ameongeza kuwa kati ya hizo zilizopendekeza na Bunge Maalum la Katiba 233 zimetokana na mapendekezo ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyowasilisha Bungeni mwezi Machi mwaka huu.
Amesema kuwa katika Ibara 47 kati ya zote za Tume 47 hazikufanyiwa marekebisho  badala yake zilibaki kama zilivyopendeza wakati Ibara  186 ndio zilifanyiwa maboresha na marekebisho kwa ajili ya kuziboresha na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba.
Mhe. Chenge ameongeza Bunge hilo limeongeza Ibara  41 mpya na kufuta 28 zilizopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Rasimu ya Katiba inayopendekeza na Bunge Maalum la Katiba ina sura mpya mbili mpya  ambayo ni ardhi ,maliasili na mazingira na sura inayohusu Serikali ya Mapinduzi ya Mapinduzi, Baraza la Mapinduzi na Baraza la Mawakilishi.

No comments:

Post a Comment