Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Bw. Makongoro Nyerere
Na Benjamin Sawe, Bagamoyo
TAASISI ya Sanaa Bagamoyo imeaswa kuendelea kutoa mafunzo
ya sanaa na utamaduni ambayo yatakidhi
mahitaji ya soko kwa nchi za Afrika
Mashariki.
Hayo yamesemwa
na Bw. Makongoro Nyerere kwa niaba ya Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mh. Margaret
Ntantongo Zziwa katika Ufunguzi wa Tamasha la 33 la sanaa na utamaduni wa
Mtanzania lililofanyika katika Taasisi hiyo mjini Bagamoyo jana
Bwana
Makongoro alisema Sanaa na Utamaduni vinaweza
kutumiwa kuelezea masuala yote yanayomuhusu binadamu na mazingira yake
hususani suala zima la utaliii
Alisema
ni wakati mwafaka kwa jamii kuondokana na dhana ya kuona watalii ni wale wa
kutoka nje ya nchi na kusahau kuwa wale wa ndani ambao kwa idadi kubwa ni wengi
wa kuwezesha Serikali kukusanya maduhuli ya kutosha.
Kwa
upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa TaSUBa Bw. Michael Kadinde alisema sanaa
hutumika kuelimisha jamii katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na Utawala Bora, kuhifadhi mazingira, madahara
ya rushwa katika jamii, namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Ukimwi na aina nyingine nyingi za utoaji elimu
katika jamii.
Alitolea
mfano wa sanaa ya ngoma, nyimbo, hadidhi simulizi, majigambo, uchoraji na sanaa nyingine nyingi za makabila mbalimbali
vinaeleza utamaduni wa Mtanzania hivyo huwa kitambulisho cha jamii.
Bw.
Kadinde alisema sanaa huonya na kutaadhalisha jamii juu ya mambo mabaya
yanayoweza kuleta madahara katika jamii ikiwa ni pamoja na kuendekeza rushwa, Vijana
au jamii nzima kuwa na tabia zisizokuwa
na heshima .
Aliomba
Bodi ya Utalii ya Tanzania mahali palipo na vituo vya Utalii viwatumie wahitimu
wa TaSUBa kuanzisha vikundi vya sanaa
ili watangaze utalii wa nchi ili na kuongeza mapato ya nchi na jamii kwa ujumla.
Alisema
kutoa mafunzo ya Sanaa na Utamaduni kwa nchi za Afrika Mashariki kuna
changamoto zake ikiwa ni pamoja na upanuzi wa miundombinu ili kukidhi mahitaji
ya ufundishaji ambapo iliyopo haiwezi kubeba mzigo mzito wa kutoa mafunzo kwa
wanafunzi wa nchi za Afrika Mashariki.
Tamasha la sanaa Bagamoyo lilianzishwa mwaka 1982
ambapo mwaka huu kauli mbiu yake ni “Sanaa
na Utamaduni katika kukuza utalii”.
No comments:
Post a Comment