Baadhi ya viongozi wa Dini waliofuatana na Sheikh Hemed Jalala wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba (hayupo pichani). Wa kwanza kulia ni Alhaj Mohamed Mputa na anayemfutia ni Sheikh Mohamed Abdi.
Baadhi ya Waandishi wakifuatilia mazungumzo kati ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba na mgeni wake Sheikh Hemed Jalala leo 03 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
Sheikh Hemed Jalala (kushoto), akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta (wa kwanza kulia) leo 03 Septemba, 2014 mjini Dodoma.Katikati ni Mjumbe wa Bunge hilo, Mhe. Yassmin Alloo.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samuel Sitta (wa
tatu toka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Sheikh Hemed Jalala (wa pili
toka kushoto) pamoja ujumbe aliofautana nao. Wa kwanza kulia ni Alhaj Mohamed
Mputa, anayemfuatia ni Sheikh Mohamed Abdi na wa tatu toka kulia ni Mjumbe wa
Bunge hilo, Mhe. Yassmin Alloo. (Picha
zote na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma)
Na Magreth Kinabo, Dodoma.
03/09/2014.
BAADHI ya viongozi wa dini wamempongeza Mwenyekiti wa
Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta kwa kitendo chake cha kuliendesha Bunge hilo vizuri katika hali ya utulivu na amani.
Kauli hiyo imetolewa leo na Sheikh Hemed Jalala kutoka Msikiti wa Ghadiir
uliopo maeneo ya Kigogo Post jijini Dares Salaam, ambaye aliambatana na Masheikh
wengine ambao ni Alhaji Mohamed Mputa, Sheikh
Mohamed Abdi na Masoud Mbilili.
Aidha Sheikh Jalala
akizungumza kwaniaba ya viongozi wenzake wa dini alisema kuwa wamekuja kutembelea
Bungeni hapo kwa ajili ya kumshukuru Mhe. Sitta na kumuunga mkono kwa kazi nzito
nzuri anayoifanya huku akisisitiza kuwa wako nyuma yake katika suala hilo.
“Pamoja na changamoto zilizojitokeza umeweza kukabiliananazo
vizuri. Sisi na wananchi kila tunapolifuatilia tunaona mmeweza kulipeleka vizuri.
Jambo hili ni zito linahitaji amani, utulivu na kuvumiliana,” alisema Sheikh Jalala.
Sheikh Jalala alisema wao kama viongozi wa dini,
wameona kuna changamoto ya maadili hivyo, wameandaa kitabu maalum kinachoitwa
‘Kilele cha Fasaha’.
Alisema kitabu hicho kitasaidia kutoa mchango wao kwenye
masuala ya uongozi na maadili, ambacho alikikabidhi kwa Mhe. Sitta.
Akipokea kitabu hicho, Mhe.Sitta amesema ni jambo la baraka
kwake, ambapo aliahidi kutoa taarifa juu ya jambo hilo na kukikabidhi kitabu
hiko katika Kamati ya Uongozi wa Bunge hilo.
Sheikh Jalala alisema kuna jumla ya nakala 632 ya
vitabu hivyo na vimeshakabidhiwa kwenye ofisi ya Mwenyekiti wa Bunge hilo.
Katika hatua nyingine Sheikh Jalala ameongoza dua maalum
kwa ajili ya kuliombea Bunge hilo ili liweze kuendelea kwa amani, utulivu,
busara, maelewano na upendo.
No comments:
Post a Comment