TANGAZO


Wednesday, September 3, 2014

Daktari bingwa wa ugonjwa wa Saratani ya matiti kutoka Bangalore nchini India afanya mazungumzo na Madaktari wa Hospitali ya Misheni ya Kagondo mkoani Kagera kuhusu mchakato wa ujenzi wa Kituo cha Uchunguzi wa Saratani mkoani humo


Mkuu wa Utawala wa Hospitali ya Misheni ya Kagondo,  Josue Joseph (wa tatu kulia), akitoa historia fupi ya kuanzishwa kwa hospitali hiyo. Kutoka kushoto ni Wakili, Respiucis Didace, Dk.Fred Limbanga, Profesa Pais na Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kagonda, Dk.Willbrord Shangwe, Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea James Rugemalira na Dk. Father Felix Kamugisha wa hospitali hiyo.
Profesa Pais (wa pili kulia), akiwa katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Wakili, Respiucis Didace, Dk.Fred Limbanga na Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kagonda, Dk.Willbrord Shangwe.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk. Willbrod Shangwe akimwelekeza jambo Profesa Pais. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0786-858550)
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira (kulia), akizungumza na madaktari wa hospitali hiyo wakati akimtambulisha Profesa Pais. Profesa Pais yupo nchini kwa mualiko maalumu na James Rugemalira. Kushoto Mkuu wa Utawala wa hospitali hiyo, Josue Joseph.
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira (wa pili kulia) akimuelekeza jambo Mhasibu Mkuu wa Hospitali hiyo, Sister Godeberter Gosbert. Kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Willbrod Shangwe na Kulia ni Wakili Respicius Didace.
Profesa Pais na wenyeji wake wakipata maelezo kutoka kwa ofisa wa Idara ya Viungo Bandia, Salvatory Kalimanzira (kushoto), walipotembelea idara hiyo.
Profesa Pai na wenyeji wake wakipata maelezo walipotembelea maabara ya hospitali hiyo.
 Baadhi ya majengo ya wodi za hospitali hiyo.
Hali ya Mandhari ya Shule yanavyoonekana.
Profesa Pais (wa tatu kulia) na wenyeji wake wakitembelea hospitali hiyo ambayo ni tegemeo kubwa kwa wananchi wa mkoa wa Kagera kwa utoaji wa huduma bora.

No comments:

Post a Comment