TANGAZO


Saturday, September 20, 2014

CCM kuanza kuwatimua viongozi wavivu, wasio na kazi na wala rushwa


 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Mlandizi, Kibaha Vijijini, ambapo alisema kua CCM itaanza kuwafukuza viongozi wabovu na wala rushwa. Kinana yupo mkoani Pwani kuimarisha uhai wa chama, kuhimiza, na kusukuma utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM. (Picha zote na Richard Mwaikenda)
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia kaaikia wananchi kuhusu tika mkutano wa hadhara Mlandizi, Kibaha Vijijini, ambapo aliwananga wapinzania kwamba wanahangaika na maandamano wakati CCM wanahangaikia mandeleo ya wananchi.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani, Mwinshehe Mlao wakiondoka baada ya kufungua jengo la CCM Wilaya Kibaha Vijijini.
Kinana akisaidia kupaka rangi alipokagua jengo la Baraza la Ardhi la Kata ya Mlandizi lililojengwa kwa msaada wa Euphresia Kadala (kushoto), Diwani wa Kata hiyo.
Kinana akihutubia baada ya kufungua jengo la Baraza la Ardhi la Kata ya Mlandizi
Kinana akipanda mti wa kumbukumbu alipotembelea Kituo cha Afya cha Mlandizi.
Kinana akizungumza baada ya kushiriki ujenzi wa jengo la kuhifadhia maiti katika Kituo cha Afya cha Mlandizi.
Kinana akipandisha bendera wakati wa uzinduzi wa shina la wakereketwa wa Kikundi cha Mshikamano Mlandizi Mjini.
Nape akimbusu mtoto Ashrafu Waziri, mkazi wa Mlandizi wakati wa ziara kuimarisha uhai wa chama Kibaha Vijijini.
Wafuasi wa CCM, wakisikiliza kwa makini wakati Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akihutubia katika uzinduzi wa shina la vijana la mshikamano Kibaha Vijijini. Kutoka kulia ni Flaviana Juma, Moureen Willfred na Fadhila Jumanne.
Kinana akikagua mradi wa maji katika Kijiji cha Bokomnemela Kibaha Vijijini.
 Kinana akiagana na Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dk. Hashim Mohamed baada ya kukagua mradi wa maji katika Kijiji cha Bokomnemela. 
Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani, Joyce Masunga akihutubia katika mkutano huo.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa akielezea kuhusu miradi mbalimbali iliyotekelezwa katika jimbo hilo kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Mkazi wa Mlandizi akiuliza swali katika Mahakama ya wazi ya Kinana katika kutano huo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza akijibu swali la mwananchi aliyelalamikia kitendo cha waalimu kuwafukuza wanafunzi waliokosa kutoa michango shuleni ambapo Kinana alikemea vitendo hivyo.
 Baadhi ya wanachama wa Chama cha Chadema wakionesha kadi zao wakati wakizirejesha na kujiunga na CCM katika mkutano uliofanyika Kibaha Mlandizi.
Wanachama wapya wakila kiapo baada ya kukabidhiwa kadi za chama  hicho.

No comments:

Post a Comment