Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema akitoa ufafanuzi wa masuala
Kisheria kwa waandishi wa habari kuhusu
mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini
Dar es Salaam.
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema akiwaonesha waandishi wa habari Rasimu
ya katiba wakati akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kisheria katika
mchakato wa Katiba wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema akiwaonesha waandishi wa habari Rasimu
ya katiba wakati akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kisheria katika
mchakato wa Katiba wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick
Werema wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Hassan
Silayo)
Na Rose Masaka-MAELEZO
Viongozi wa vyama vya siasa
waliopo nje ya Bunge Maalumu la Katiba wameaswa kurejea bungeni ili kufanya maridhiano
ndani ya bunge hilo.
Kauli hiyo imetolewa na
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alipokuwa akiongea na waandishi
wa habari leo Jijini Dar es Salaam.
Jaji Werema amesema kuwa
wajumbe walio nje ya Bunge Maalum hawana budi kurejea bungeni na kuacha kumshinikiza
Rais kulivunja bunge hilo kwani hana mamlaka ya kulivunja kulingana na sheria inayoliongoza
bunge hilo.
“Sheria inasema kuwa baada
ya bunge hilo linaweza kuvujwa baada ya katiba kupatikana, kinyume na hapo
bunge husitishwa kufikia maridhiano na kufikia mwafaka kwa kufuata misingi ya demokrasia.”
alisema Jaji Werema.
Pia Jaji Werema alisema
kuwa wajumbe walio nje ya bunge hilo hawana budi kurudi ili kuendelea kujadili
vipengele vingine vya rasimu ili kuweza kupata katiba iliyo bora kwa nchi na
watu wake.
Aidha, Jaji Werema aliviasa
vyombo habari kutumia nafasi yao ya kuwa mhimili muhimu katika uongozaji wa
nchi kutokuwa na upendeleo katika utoaji wa taarifa na kuacha kuongozwa na
mawazo ya wachache ili kuweza kusaidia nchi kupata Katiba Mpya kwa manufaa na
maendeleo ya nchi.
No comments:
Post a Comment