Idara ya Ulinzi nchini Marekani
imesema kuwa mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Marekani
yameharibu magari mawili ya wapiganaji karibu na mlima Sinjar kazkazini
mwa Iraq.
Taarifa hiyo imesema kuwa mashambulizi hayo
yanafuatia ripoti za mashambulizi yaliotekelezwa na wapiganaji wa
Islamic State dhidi ya raia katika kijiji cha kawju.Awali,maafisa wa kikurdi wamesema kuwa vikosi vya Islamic State viliwauawa wanachama 80 wa Yazidi katika kijiji hicho cha kazkazini mwa taifa hilo ijapokuwa haikuelezea iwapo kilikuwa kijiji cha Kawju.
Msemaji wa Islamic State amesema kuwa watu wa Yazidi wanaoishi katika maeneo wanayodhibiti wana uwezo wa kubadili dini, kuondoka ama kuuawa.
No comments:
Post a Comment