Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi Juliana Yassoda (Katikati) akiongea na Wanahabari (Hawapo pichani) kuhusu makocha wa Timu ya Barcelona kutoka nchini Hispania ambao wako nchini kwa ajili ya mafunzo ya makocha yatakayofanyika kwa muda wa siku mbili, wa kwanza kulia ni Balozi wa Spain nchini Mh. Luis Manuel Ceuesta Civis, mafunzo hayo yanatolewa kwa ushirikiano na Kiwanda cha Bia cha Tanzania Breweries.
Kocha Isaac Oriol Guerrero Hernandes (katikati) kutoka timu ya Barcelona ya nchini Hispania (katikati) akitoa maelezo kwa wanahabari (hawapo pichani) kuhusu mafunzo ya siku mbili watakayotoa kwa makocha 30 wakizalendo, kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Bi. Juliana Yassoda na wa kwanza kushoto ni kocha Kocha Daniel Bigas Alsina.
Makocha wa Kizalendo 30 ambao
wanatarajiwa kupewa mafunzo ya siku mbili kutoka kwa makocha wa Barcelona
wakiwa katika picha ya pamoja. (Picha zote na Benjamin
Sawe kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WHVUM)
Na Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalini, WHVUM
Tarehe: 01/08/2014
SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni, na
Michezo imewataka Makocha wa Mpira wa Miguu wanaopata mafunzo ya siku mbili kutoka
kwa makocha wa Timu ya FC Bacelona waliotoka Spain kuinua mchezo wa Mpira wa
miguu hivyo kuitangaza nchi ya Tanzania kimataifa.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya
Michezo Bibi. Juliana Yassoda wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Makocha 30 wa
Mpira wa Miguu yaliyoandaliwa na Tanzania Brweweries Limited kupitia kinywaji
cha Castle Lager leo jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Karume.
Bibi. Yassoda amesema kuwa Wizara inatamani kuona
wachezaji, klabu pamoja na timu za taifa kuwa katika nyanja ya kimataifa kwani
michezo ni shughuli za kiuchumi, kimichezo na kijamii haswa mpira wa miguu unaovutia
duniani kote.
Akitoa
wosia kwa makocha Bibi. Yassoda amewaomba washiriki kuwa makini na kuwa na nidhamu wakati wa mafunzo ili kuongeza ujuzi pia
kuwa na uhakika na serikali yao kwani serikali itaendelea kujenga mazingira mazuri na wawekezaji kiuchumi na kijamii katika sekta ya
michezo kwa manufaa ya watanzania
wote.
Aidha Balozi wa Spain
nchini Tanzania Bw. Luis Manuel Ceuesta Civis ameishukuru kampuni ya Tanzania
Breweries kupitia bia yao ya Castle Lager kuandaa mafunzo hayo kwa makocha na
kuwataka makocha wanaoshiriki mafunzo hayo kuchukua ujuzi na kanuni za mpira kutoka kwa makocha wa FC Bacelona.
Naye Mkurugenzi wa
Masoko kutoka Tanzania Breweries Limited Bi. Kushillah Thomas amewataka makocha
wa Mpira wa Miguu kutoka Tanzania kupokea mafunzo maalum kutoka kwa
wataalam wanaoongoza moja ya timu zenye mafanikio zaidi duniani kwa kutumia
ujuzi mpya watakaoupata kuinua vipaji vya wachezaji na kuwaendeleza wanamichezo
kuwa wanamichezo wa kimataifa.
No comments:
Post a Comment