Meneja Uhusiano wa NDC, Bw. Abel Ngapemba
Frank
Mvungi-Maelezo
Serikali kutumia
Euro Milioni 16 katika ujenzi wa Kiwanda cha kuzalisha viuadudu vinavyoua
viluwiluwi vya mbu wanaoambukiza malaria ulioko chini ya shirika la Taifa la
Maendeleo (NDC) unaotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
Hayo yamesemwa
na Meneja Uhusiano wa Shirika hilo Bw. Abel Ngapemba wakati wa mkutano
nawaandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam.
“Hivi sasa
majengo yote yamekwisha kamilika katika eneo la Maili moja Kibaha Mkoani Pwani
na mitambo yote imeshawasili na wataalamu wanaifunga ambapo kabla ya mwisho wa
mwaka uzalishaji wa majaribio utaanza” Alisema Ngapemba.
Akifafanua zaidi
Ngapemba alisema kiwanda hicho kitasaidia kuzalisha ajira za moja kwa moja zipatazo 172 kwa watanzania.
Pia Ngapemba
alibainisha kuwa kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha lita milioni sita
za viadudu kwa mwaka ambapo asilimia 80 ya dawa hizo zitatumika nchini na
asilimia 20 zitauzwa nchi za nje ambazo tayari zimeonyesha nia ya kuzitaka dawa
hizo.
Viadudu hivyo
vinatengenezwa kutokana na vimelea ambao wanakuzwa kwa kutumia viinilishe
mbalimbali na kunyinyiziwa katika maeneo yenye mazalia ya mbu ambapo viluwiluwi
wa mbu wanapovila wanakufa.
Kulingana na
ripoti ya upembuzi yakinifu wa mradi huu uliofanywa na NDC kwa kushirikiana na kampuni
ya Labiofam ya Cuba mwaka 2010, mbali na malaria kusababisha vifo vya
Watanzania wapatao 80,000 kwa mwaka,ambapo watu milioni 18 huugua ugonjwa huo
kila mwaka ambapo Serikali imekuwa ikitumia kiasi cha dola za marekani zipatazo
milioni 240 kwa mwaka katika kupambana na ugonjwa huu.
Ujenzi wa
Kiwanda hicho ulianza miaka miwili iliyopita na kuwekwa jiwe la msingi na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Jakaya Mrisho Kikwete October mwaka 2013
lengo likiwa kupambana na hatimaye kutokomeza mbu wanaoeneza malaria na
magonjwa mengine yaenezwayo na mbu.
No comments:
Post a Comment