Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira (katikati), akiongea na waandishi wa habari jana, mjini Dodoma juu ya mkutano wa 30, utakaofanyika nchini mwishoni wiki hii.
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Kusini na Mashariki ya Afrika (PTA), Admassu Tadesse, akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, kuhusu mkutano wa miaka 30 ya wanahisa na magavana utakao shirikisha nchi 18 za Afrika. Mkutano huo utafanyika kesho, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Ofisi ya Rais (Uratibu na Mahusiano), Steven Wasira na kulia ni Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba.
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Kusini na Mashariki ya Afrika (PTA), Admassu Tadesse, akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, kuhusu mkutano wa miaka 30 ya wanahisa na magavana utakao shirikisha nchi 18 za Afrika. Mkutano huo utafanyika kesho, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira (kushoto), abibadilishana mawazo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Kusini na Mashariki ya Afrika (PTA), Admassu Tadesse, mara baada ya mkutano na waandishi wa habari jana, mjini Dodoma. Katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Servacius Likwelile. (Picha zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
Na Eleuteri Mangi-
MAELEZO
19/082014
Bodi ya Magavana wa
Benki ya Maendeleo ya Biashara Mashariki na Kusini mwa Afrika (PTA) itakuwa mkutano
wa mwaka utakaofanyikia nchini jijini Dar es salaam tarehe 22 mwezi huu.
Hayo yamebainishwa jana
mjini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Stephen
Wasira alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya mkutano huo
utakaofanyika mwishoni wiki hii.
“Huu ni mkutano wa
kawaida wa mwaka wa Bodi ya Magavana wa nchi wanachama pamoja na Mawaziri wa
Fedha, Tanzania ni mwanachama ndio maana mkutano wa 30 unafanyika hapa” alisema
Wasira.
Wasira amesema kuwa
katika mkutano huo mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwemo masuala ya fedha na
uchumi, maendeleo ya benki ya PTA na mafanikio yake kwa nchi washirika.
Vile vile Wasira amesema
kuwa PTA ni benki ya Kiafrika na inafanyakazi nzuri ambapo inaonesha inakua kwa
zaidi ya asilimia 30 kwa mwaka kwa miaka kadhaa hadi sasa na imekuwa na mizania
ya Dola za Kimarekani mil. 2.8 ikiwa miongoni mwa benki za maendeleo
zinazofanya vizuri katika bara la Afrika.
Aidha, Wasira ameongeza
kuwa mkutano huo utatanguliwa na semina ya wafanyabiashara itakayofanyika Agosti
21 siku moja kabla ya mkutano mkuu wa Magavana hao ambapo Serikali
itawakilishwa na Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba.
Kwa upande wake Rais na
Mtendaji Mkuu wa benki ya PTA Admassu Tadesse amesema kuwa Tanzania imekuwa
mstari wa mbele na ni mwanachama hai ambapo imekuwa mfano mzuri kwa nchi
wanachama kwa kutoa michango mbalimbali kwa wakati.
Zaidi ya hayo, Tadesse
amesema kuwa benki hiyo mwaka huu inaadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwake,
Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa mkutano wa mwaka huu ili
washerehekee na Watanzania.
Tadesse amesisitiza kuwa
Benki ya PTA inatoa huduma zake kwa nchi wanachama ikiwa na lengo la kuwa
tasisi ya kifedha inayoongoza Mashariki na Kusini mwa Afrika katika utoaji wa
huduma za kibenki.
Benki ya PTA
ilianzishwa mwaka 1985 ambapo hadi sasa ina jumla ya wanachama 22 ikiwemo nchi
18 ambazo ni Burundi, Comoros, Djibouti Congo, Kenya na Malawi.
Nchi nyinine ni Misri, Eritrea,
Ethiopia, Mauritania, Rwanda, Seychelles, Somalia, Sudan, Uganda, Zambia, Zimbabwe
na mwenyeji Tanzania
Aidha, PTA
inashirikiana na nchi nyingine nje ya bara la Afrika ambazo ni Belarus na China.
Washirika wengine ni Benki
ya Maendeleo ya Afrika (ADB), Kampuni ya Bima ya Mauritia iitwayo Eagle na
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Mauritius.
Mkutano wa mwaka huu
unafanyikia Tanzania ikiwa ni utaratibu wa benkiya PTA kufanya mikutano ya
mwaka kwa mzunguko ambapo washiriki watakuwa Mawaziri wa Fedha, Magavana wa
nchi wanachama, sekta binafsi, Mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali nchini
na Wawakilishi wa Mashirika ya kimataifa.
No comments:
Post a Comment