Rais wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi
Na
Joseph Ishengoma, Maelezo
RAIS
wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi amesema serikali haijawahi kufuta
Azimio la Arusha kama inavyodaiwa na baadhi ya wananchi, bali ilizimua azimio
hilo kuwapatia viongozi wa kati uwezo wa kumudu makali ya maisha.
“Serikali
haikufuta Azimio la Arusha. Ililizimua azimio hilo kuwapatia viongozi wa kati
kumudu makali ya maisha, lakini baadhi ya viongozi wamekuwa wakitumia vibaya
nafasi hiyo kuvunja sheria ya maadili ya viongozi,” amesema.
Alhaji
Mwinyi ameeleza hayo leo jijini Dar es Salaam katika semina ya siku moja ya
maandalizi ya sheria ya kudhibiti mgongano wa maslai miongoni mwa viongozi na
watumishi wa umma iliyoandaliwa na Sekretarieti ya Maadili ya viongozi.
“Baadhi
ya watu wamekuwa wakitumia vibaya nafasi hiyo kuvunja maadili ya viongozi wa
umma kwa kutumia raslimali za umma kujinufaisha. Tabia hii imewafanya wananchi
kutokuwa na imani na viongozi wao,” amesema.
Kwa
mujibu wa Alhaji Mwinyi, mgongano wa maslai ini tatizo kubwa nchini
linalotakiwa kuangaliwa kwa umakini vinginevyo baadhi ya viongozi wataendelea
kujinufaisha kwa kutumia nafasi zao kazini.
Kwa
upande wake Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya viongozi Jaji Salome Kaganda
amesema lengo na makusudi ya mapendekezo ya sheria hii ni kuleta amani na
utulivu wan chi.
Jaji
Kaganda amesema, “mapendekezo ya sheria hii hayalengi kuwafanya viongozi kuwa
maskini, bali kasi yao ya ukwasi iendane na halii halisi ya kipato chao.”
“Sheria
hii itakapopitishwa na ngazi husika, itapunguza ubinafsi wa viongozi walioko
madarakani kujipendelea wenyewe na maeneo wanayotoka,” amesema na kuongeza
kuwa, “Lazima kuwepo na hatua uya serikali kurejesha maadili ya maadili. Kama itazingatiwa
na kuheshuimiwa, taifa litafikia maendeleoo ya haraka yaliyokusudiwa.”
No comments:
Post a Comment