TANGAZO


Friday, July 4, 2014

Wanamichezo waliokuwa China kujiandaa na Mashindano ya Jumuiya ya Madola warejea nchini huku wakiwa na matumaini makubwa

Baadhi ya wanamichezo waliokuwa nchini China kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Jumuiya ya Madola wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo, jijini Dar es Salaam .
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini Bw. Leonard Thadeo akisukuma mzizigo ya baadhi ya makocha wa China waliombatana na Wanamichezo wa Tanzania waliokuwa China kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa na mashindano ya Olympic yanayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu mjini Glasgow Scotland, Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Bibi. Juliana Yassoda akimpokea mmoja wa wanamichezo hao mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Msafara wa Makocha sita kutoka China Bw. Kangkai akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa  Julius Nyerere.Makocha hao wa kutoka China ndiyo ambao walikuwa wakiwafundisha wachezaji wa michezo ya Riadha, Ngumi na Mpira wa Mezani (Table Tennis) wanamichezo wa Tanzania waliokwemda nchini humo kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Olympic mjini Glasgow Scotland.
Mkuu wa msafara wa wanamichezo kutoka Tanzania waliokuwa nchini China kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Olympic Bw. Boniphace Kimisha akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo. 
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bw. Leonard Thadeo akizungumza na wanamichezo waliokuwa nchini china kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Olympic, mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo. 
Makocha sita kutoka China waliombatana na timu ya wanamichezo wa Tanzania waliokuwa wameenda nchini China kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Olympic yanayotaraji kuanza mapema mwishoni mwa mwezi huu mjini Glasgow Scotland. Makocha hao wanafundisha michezo ya Riadha, Ngumi na Table Tenisi.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini Bw. Leonard Thadeo (wapili kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji na makocho kutoka china mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo nchini Bibi. Juliana Yasoda (mwenye gauni la kitenge) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji na makocho kutoka china mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Frank Shija, Kitengo cha Mawasiliano Serikalin - WHVUM)

No comments:

Post a Comment