TANGAZO


Friday, July 4, 2014

Mama Salma Kikwete atembelea Maonesho ya Biashara ya Kimataifa, Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Barabara Kilwa, jijini Dar es Salaam

Mke wa Rais Mama  Salma Kikwete (katikati mwenye kitenge), akitembelea leo  maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea  kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam. Kulia  ni  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema.
Mke wa Rais Mama  Salma Kikwete (katikati mwenye kitenge), akipata  maelezo  leo kuhusu bidhaa mbalimbali  kutoka kwa Bi. mkubwa  Juma kwenye banda la Zanzibar  katika maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea  kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dares Salaam.Kushoto  ni  Mkuu wa Wilaya ya Temeke,  Sophia Mjema.
Mke wa Rais Mama  Salma Kikwete (katikati mwenye kitenge), akipokelewa  na mke wa Rais wa Awamu ya Tatu, Mama Anna Mkapa wakati alipotembelea leo, maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam. Kulia  ni  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema.
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete akisaini kitabu cha wageni  wakati alipotembelea leo, banda la mke wa Rais wa Awamu ya Tatu, Mama Anna Mkapa kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama, Salma Kikwete akiangalia aina za ungo   wakati alipotembelea leo, banda la mke wa Rais wa Awamu ya Tatu, Mama Anna Mkapa kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya sabasaba, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema.
Mke wa Rais Mama, Salma Kikwete akipata maelezo kuhusu vitabu vya mchakato wa Rasimu ya Katiba mpya na vya sheria kutoka kwa Theresia Kinabo (aliyenyoosha mkono), ambaye ni Ofisa Tawala wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), na pembeni yake ni Benadeta Thomas amabye ni Ofisa Sheria wakati alipotembelea leo, banda la mke wa Rais wa Awamu ya Tatu Mama Anna Mkapa kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama  Salma Kikwete  akiangalia aina ya simu Nokia 105 katika  banda la Vodacom   wakati alipotembelea leo kwenye  maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea  kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiandika namba atakayohitaji kutumia baada ya kuchagua simu aina ya Nokia 105 katika  banda la Vodacom wakati alipotembelea leo kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea  kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama  Salma Kikwete akipata maelezo ya simu na bidhaa nyingine  katika banda la Vodacom  kutoka kwa Ofisa Mauzo  wa banda hilo, Blanca Mashoko wakati alipotembelea leo kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam. 
Mke wa Rais Mama  Salma Kikwete akisaliamiana  na Balozi wa Italia nchini, Luigi Scotto kwenye banda la Tanzania wakati alipotembelea leo, kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipata maelezo ya kikapu kidogo cha shanga cha kutunzia vifaa vya urembo kutoka kwa Cristina Kivuyo, kwenye banda la Pride mshiki kutoka Arusha   wakati alipotembelea leo, kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Magreth Kinabo- Maelezo)

No comments:

Post a Comment