Ofisa Mawasiliano
Kutoka TACAIDS Bw. Godlease Malisa akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo
pichani) wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika banda la
TACAIDS kwenye viwanja vya Sabasaba leo, jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkurugenzi
wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania, Dk. Jerome
Kamwela.
Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dk. Jerome Kamwela akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika banda la TACAIDS kwenye viwanja vya Sabasaba leo, Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa Mawasiliano Kutoka TACAIDS, Bw. Godlease Malisa.
Mkurugenzi wa
Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dk. Jerome Kamwela
kati akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa wa Ufuasihii wa dawa na huduma za
jamii wa
ICAP Globali Health Action Bi. Agnes Rubare Rwegasha alipotembelea banda
la ICAP. Kushoto ni Ofisa Mawasiliano Kutoka TACAIDS, Bw. Godlease Malisa
Mkurugenzi wa
Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dk. Jerome
Kamwela akimuuliza swali Mwelimisha Rika kutoka PSI (Population Service
International) Bi. Veronica Mbilinyi alipotembelea banda hilo katika Viwanja
vya Sabasaba leo jijini Dar es Salaam. (Picha
zote na Genofeva Matemu)
Na Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikali -
WHVUM
TAFITI
zilizofanywa na Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania zinaonyesha kuwa maambukizi mapya
ya Virusi vya Ukimwi nchini yamepungua hadi kufikia asilimia 5.1 kwa mwaka
2011/2012 ambapo asilimia 6.2 ni
wanawake na asilimia 3.8 ni wanaume.
Rai
hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tume ya
Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dk. Jerome Kamwela leo katika Viwanja vya Sabasaba
alipokutana na waandishi wa Habari katika banda la TACAIDS kuwaelezea hali
halisi ya maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi nchini.
Dk.
Kamwela amesema kuwa TACAIDS imekua ikifanya ukaguzi wa tafiti (takwimu)
zilizokusanywa katika maeneo mbalimbali nchini na kuzitathmini tafiti hizo kama
zina viwango wakiwa na lengo la kupanga mikakati itakayowawezesha kuelekeza
rasililmali ili kuondoa maambukizi mapya yanayoweza kujitokeza.
“Tafiti
zinaonyesha kuwa Mkoa wa Njombe unaongoza kwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi
kwa asilimia 14.7 ambapo Iringa ina asilimia 9.1 ya watu walioathirika na
Virusi vya Ukimwi na Mbeya ikiwa na
asilimia 9, kwa upande wa mikoa yenye kiwango cha chini cha maambukizi ya
Virusi vya Ukimwi ni Manyara na Kilimanjara ikiwa na asilimia 2 ya maambukizi
ya Virusi vya Ukimwi” amesema Dr. Kamwela.
Akizungumzia
kuhusu changamoto ambazo TACAIDS imekua ikizipata katika ukusanyaji wa takwimu
za watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi nchini Dr. Kamwela amesema kuwa uhaba wa
wataalamu, uhaba wa vyuo vinavyofundisha taaluma ya ufuatiliaji na tathmini
pamoja na uhaba wa fedha kwaajili ya kufuatilia na kutathimini hali halisi ya
maambukizi ya Ukimwi nchini vimekua vikizuia malengo ya kutokomeza Ukimwi
nchini.
Kwa
upande wake Afisa Mawasiliano kutoka TACAIDS Bw. Godlease Malisa amesema kuwa
TACAIDS imekuja na mkakati unaozingatia sifuri tatu (three zeros) ukiwa na
maana sifuri ya kwanza maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi yashuke hadi
sifuri, huku sifuri ya pili ikimaanisha unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na
Virusi vya Ukimwi upingwe hadi sifuri na sifuri ya tatu ikimaanisha maambukizi
ya mama kwenda kwa mtoto yapunguzwe hadi sifuri.
No comments:
Post a Comment