Waendesha mashitaka wa jumuiya ya Ulaya wamesema kuwa baadhi ya viongozi wa zamani wa jeshi la ukombozi la Kosovo wanastahili kufunguliwa mashitaka dhidi ya ukiukaji wa haki za binadamu.
Tuhuma wanazodaiwa kuhusishwa nazo viongozi hao wa zamani wa Kosovo ni uhalifu dhidi ya haki za binadamu,mauaji ya kikabila vitendo vinavyodaiwa kutekelezwa miaka ya 1990.
Msemaji wa waendesha mashitaka hao Clint Williamson hakutaja majina ya viongozi hao wanaostahili kushitakiwa.
Viongozi wa kundi la KLA walitwaa madaraka ya serikali ya Kosovo na kujitangazia uhuru wa taifa hilo 2008.
Washirika wa serikali ya sasa ya Kosovo akiwemo Waziri Mkuu Hashim Thaçi awali walikanusha tuhuma zilizokuwa tajwa kuwahusisha kuhusiana na vitendo vya ukatili wa kibinadamu vilivyofanyika.
No comments:
Post a Comment