*Zamu hii ni la kuwa Nyota wa Demokrasia Afrika
Rais Jakaya Kikwete
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa mara
nyingine ametunukiwa tuzo la kimataifa – zamu hii kwa kuwa mshindi waTuzo la
Nyota wa Demokrasia Afrika 2014 – Icon
of Democracy Award Winner for 2014 in Africa.
Kwa
mujibu wa barua aliyoandikiwa Rais Kikwete na kupokelewa Ikulu, Dar Es Salaam,
Rais Kikwete amekuwa mshindi wa kwanza, na kwa mbali kabisa, katika mchuano na
marais watatu wa Afrika ambao walifikia mwisho mwa mchuano wa kuwania tuzo
hilo.
Katika
barua hiyo, Mchapishaji na Mhariri Mkuu wa Jarida hilo, Pastor Elvis Iruh,
akizungumza kwa niaba ya Kamati ya Tuzo 2014, amesema kuwa uongozi wa Rais
Kikwete umekuwa ni hadithi ya kusifiwa ya mafanikio katika Bara ambako hadithi
za namna hiyo siyo nyingi.
Tuzo
hilo hutolewa na Jarida la The Voice na mwaka jana mshindi
alikuwa ni Rais Bai Koroma wa Sierra Leone ambaye alikuwa ni mshindi wa pili wa
Tuzo hiyo ambalo ilitolewa kwa mara ya kwanza kwa Rais wa Kwanza wa Zambia,
Mzee Kenneth Kaunda.
Sherehe
maalum ya kukabidhi tuzo hiyo imepangwa kufanyika Oktoba 17, mwaka huu, 2014,
katika Hoteli ya Van der Valk, iliyoko Almere, Uholanzi.
Miongoni
mwa sifa nyingine, Rais Kikwete anatunukiwa Tuzo hiyo kwa sababu ya kuwa
msimamizi mzuri na wa kweli wa demokrasia, kuendelea kuhakikisha kuwa amani,
utulivu na maendeleo vinaendelea kupatikana katika eneo la Afrika ambalo
limepitia vipindi vingi vya migogoro na matatizo.
Aidha,
gazeti hilo linasema kuwa Rais Kikwete amekuwa kiongozi wa mfano, kimataifa na
kikanda, na linatoa mfano wa mchango wake katika kusuluhisha mgogoro mkubwa wa
kisiasa nchini Kenya kufuatia uchaguzi mkuu wa 2007.
Rais
Kikwete pia anasifiwa kwa mchango wake katika kusimamia maendeleo ya Tanzania
katika nyanja mbali mbali – kilimo, elimu, miundombinu, maendeleo ya viwanda,
utalii na pia mchango wake katika kuendeleza vijana na kutoa nafasi nyingi kwa
akinamama kushika nafasi nyingi za uongozi.
Jarida
la The
Voice pia limempongeza Rais Kikwete kwa kuimarisha Umoja na Muungano wa
Tanzania na kutoa nafasi kwa wananchi kujadili na kukubaliana kuhusu Katiba
mpya ya Tanzania.
Aprili
mwaka huu, Rais Kikwete alitunukiwa tuzo la kuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa
zaidi katika maendeleo ya Afrika kwa mwaka 2013 – The Most Impactful Leader in
Africa 2013.
Imetolewa
na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
30
Julai,2014
No comments:
Post a Comment