Mwanamume mmoja aliyezuiwa katika kituo cha wagonjwa wa akili kwa kutomuamini Mungu amechiliwa huru.
Mubarak Bala alifungwa kutokana na mzozo
uliozuka huko Kano kaskazini mwa Nigeria baada ya ripoti kwamba ameuasi
uislamu na kujitangaza kuwa mtu asiyeamini Mungu.Alifungwa kwa siku kumi na nane katika taasisi hiyo ya watu wenye magonjwa ya akili katika jimbo la Kano baada ya jamaa zake kumpeleka huko kwa lazima.
Aliuasi uislamu na kujitangaza mtu aisyeamini kwamba kuna Mungu.
Mubarak Bala ameeleza kwamba babake alikuwa kiongozi wa dini ya kiislamu ambaye hangekubali kuwa na familia iliyo na waumini wasio waislamu.
Kuna taarifa kwamba aliachiliwa kutoka kituo hicho cha afya, kutokana na mgomo wa kitaifa wa madakatari. Lakini inaonekana matatizo yanayomkumba Mubarak Bala hayajamalizika.
Amepokea vitisho vya kumuua kwa kuritadi uislamu, na anasema licha ya kuwa anataka kurudi kuwa na familia yake, anataka pia kuondoka katika eneo hilo la kaskazini lenye idadi kubwa ya waislamu.
Dini ni kitu kizito kukijadili Nigeria, hususan wakati wapiganaji wenye itikadi kali ya dini ya kiislamu wanapigana kuidhinisha jimbo la kiislamu.
No comments:
Post a Comment