Aliyekuwa mhariri wa
gazeti moja nchini Uingereza Andy Coulson ambaye baadaye alihudumu kama
mshauri wa waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amehukumiwa kifungo
cha miezi 18 gerezani kwa makosa ya udukuzi wa mawasilioni ya simu.
Wiki iliyopita Coulson alipatikana na hatia ya kudukuwa mawasiliono ya simu alipokuwa mhariri wa gazeti la News of the World.Gazeti hilo baadaye lilifungwa kutokakana na shinikizo kutoka kwa umma nchini Uingereza kufuatia kashfa hiyo ambapo simu za famiia za kifalme, za wanasiasa, za watu mashuhuri na watu wa kawaida zilidukuliwa.
Kufutia hukumu hiyo, waziri mkuu wa Uingereza aliomba msamaha kwa kumteua Coulson kuwa mshauri wake.
Waandishi wengine wa zamani na mchunguzi wa kibinafsi Glenn Mulcaier walikiri kufanya udukuzi wa mawasiliono ya simu na walipewa hukumu ndogo.
No comments:
Post a Comment