TANGAZO


Sunday, July 6, 2014

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi atembelea Zahanati iliyokataliwa na Waziri Mkuu Pinda

*Aagiza Manispaa ya Dodoma kutoa kipaumbele kwa Zahanati ya Mkonze

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi (katikati) akizungumza na baadhi ya Viongozi wa kijiji cha Mkonze, wajumbe wa kamati ya Afya kijijini hapo, na baadhi ya watumishi wa Manispaa ya Dodoma mapema juzi Julai 3, wakati alipotembelea Zahanati ya Kijij hicho kukagua ukarabati wa jengo la zahanati
ya kijiji, lililokuwa limeathirika kwa kufanya nyufa kwenye baadhi ya kuta na kusababisha rasilimali hiyo, ya Serikali isitumike kutoa huduma kwa wananchi kwa sababu za kiusalama.

Jengo la Zahanati ya Kijiji cha Mkonze, Manispaa ya Dodoma, likiwa limeanza kujengewa nguzo kwenye kuta kwa lengo la kuliongezea uimara. Jengo hilo, lililokuwa limeathirika kwa kufanya nyufa kwenye baadhi ya kuta na kusababisha rasilimali hiyo, ya serikali isitumike kutoa huduma kwa wananchi kwa sababu za kiusalama.
Jengo la Zahanati ya Kijiji cha Mkonze, Manispaa ya Dodoma, lililokuwa limeathirika kwa kufanya nyufa kwenye baadhi ya kuta na kusababisha rasilimali hiyo, ya serikali isitumike kutoa huduma kwa wananchi kwa sababu za kiusalama kwa sasa linafanyiwa ukarabati kwa kuanzia na kujengewa nguzo ili kulipa uimara na kuondoa mapungufu yaliyojitokeza ili jengo hilo, lianze kutoa huduma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi akikagua nguzo zilizojengwa kwa lengo la kuongeza uimara kwenye jengo la Zahanati ya Kijiji cha Mkonze, Manispaa ya Dodoma lililokuwa limeathirika kwa kufanya nyufa kwenye baadhi ya kuta na kusababisha rasilimali hiyo, ya Serikali isitumike kutoa huduma kwa wananchi kwa sababu za kiusalama. Mkuu huyo wa Mkoa alifanya ziara hiyo mapema juzi, Julai 3. (Picha zote na John Banda, Dodoma)

Na John Banda, Dodoma
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Rehema Nchimbi amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, kuhakikisha anatoa kipaumbele cha mradi wa ujenzi wa zahanati ya Mkonze na kuhakikisha ukarabati wa jengo hilo unakamilika mara moja
ili ianze kutoa huduma kwa wananchi.

Nchimbi alitoa agizo hilo baada ya kutembelea katika kjiji hicho cha Mkonze kilichopo Manispaa ya Dodoma na kujionea  zahanati hiyo ilivyojengwa chini ya kiwango na kuamuru ukarabati ufanyike kitaaramu.

Alisema Mkurugenzi wa manispaa na timu yake wahakikishe wanatoa kipaumbele katika marekebisho ya ujenzi wa jingo hilo ambalo kuta zake zimeweka nyufa kabla hata ya kuanza kutumika.

Alisema mradi huo unaonyesha kulikuwa na hali ya kulegalega kwenye utekelezaji na usimamizi wa ujenzi wa jingo hilo na hata wataaramu hawakufanya kazi yao ipasavyo ndiyo maana imejitokeza athari kama hizo.

Awali akisoma Risala kwa niaba ya wananchi Yusufu Jacob aliulalamikia usimamizi mbovu  wa utekelezaji wa mradi huo hali ilisababisha changamoto hizo zinazochelewesha huduma kwa wananchi ambao wamekuwa wakifuata huduma za afya mjini kwa umbali mrefu hali inayowasababishia adha kubwa.

Siku za nyuma, Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliwahi kutembelea mradi huo mapema mwezi Machi mwaka huu na kujionea dosari hizo kwenye jengo hilo na kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa Dodoma na timu yake ya Watendaji kulifanyia haraka ukarabati jengo hilo, ili lianze kutoa huduma lakini aliporudi mwezi Juni kuangalia utekelezaji wa maelekezo yake, alikuta hali isiyoridhisha na kuagiza lisifunguliwe mpaka litakapokamilika,
hivyo kujitokeza ujenzi huo wa zahanati unaonekana haukuwa na usimamizi wowote.

No comments:

Post a Comment