TANGAZO


Sunday, July 6, 2014

Rais Kikwete, wananchi walivyotembelea Maonesho ya Biashara ya Kimataifa, Viwanja vya Malimu Nyerere Dar es Salaam

Rais Jakaya Kikwete akipatiwa maelezo na mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Veta, Eliudi Urasa (kushoto), kuhusu mfano wa injini ya ndege iliyotengenezwa na chuo hicho, wakati alipotembelea banda la Veta katika maonesho hayo, Dar es Salaam leo. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Rais Jakaya Kikwete akipatiwa maelezo na Mkuu wa Kitengo cha Mikopo ya Wajasiriamali wadogo na wa kati wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (kulia), wakati alipolitembelea banda la benki hiyo, katika maonesho ya Biashara ya Kimataifa, viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam jana.
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akisaini kitabu cha wageni huku akipatiwa maelezo ya huduma zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kutoka kwa Meneja Mawasiliano, Habari na Masoko wa mfuko huo, Constatina Martin, alipotembelea banda hilo katika maonesho hayo jana.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Kampuni ya Watumishi Housing, Weja Luto (kushoto), akiwapatia maelezo wananchi waliotembelea banda la kampuni hiyo, leo katika maonesho ya Biashara ya Kimataifa kuhusu kazi na wajibu wa kampuni hiyo katika ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma. 

Mwanafunzi wa Chuo cha Diplomasia cha Dar es Salaam, Dunga Omar (kushoto), akiwapatia maelezo wananchi, kuhusu Siwa na kazi za Bunge la Tanzania, wakati walipotembelea banda la Bunge katika maonesho ya Biashara ya Kimataifa jijini leo.

No comments:

Post a Comment