TANGAZO


Tuesday, July 29, 2014

Makamanda wa Kosovo washtakiwe - Ripoti

Wanajeshi wa Jeshi la Kosovo

Mwendesha mashtaka kutoka kwa Jumuia ya Ulaya amesema baadhi ya viongozi wa zamani wa Jeshi la ukombozi la Kosovo, Kosovo Liberation Army wanapaswa kufunguliwa mashtaka ya makosa dhidi ya binadamu ikiwemo mauaji, kuweka kizuizini watu kinyume cha sheria.
Clint Williamson alitumia miaka mitatu akifanya uchunguzi kuhusiana na mauaji kufuatia machafuko yaliyotokea Kosovo katika miaka 1990.
Hadi hapo baadae kwa sasa hatawataja waliohusika mmoja mmoja kwa sababu wengi wao wameshika madaraka serikalini.Amesema kuna ushahidi wa kutosha wa kuandaa mashtaka mara tu mahakama maalum itakapoanzishwa.
Tuhuma za kukata viungo vya binadamu na kuvisafirisha ni miongoni mwa makosa wanayotuhumiwa lakini hata hivyo makosa hayo ni kwa kiwango fulani.
Uchunguzi huo ulianzishwa kufuatia ripoti yenye utata iliyoandaliwa na baraza la Ulaya miaka minne iliyopita, iliyosema kuwa wakuu katika uongozi wa sasa nchini Kosovo akiwemo waziri mkuu Hashim Thaci, walihusika na biashara ya viungo vya miili ya binadamu kutoka kwa waserbia nchini Kosovo.
Hata hiyo wote hao wanakana kutenda makosa hayo.

No comments:

Post a Comment