TANGAZO


Tuesday, July 29, 2014

Israel yaendeleza mashambulizi makali

Mabaki ya vifusi baada ya mashambulizi katika eneo la Gaza
Israel imeendeleza mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Hamas katika eneo la Gaza baada ya mashambulizi makali ya mabomu iliyoyafanya usiku wa kuamkia Jumanne yanayohesabika kuwa ni makali tangu operesheni ya kupambana na Hamas iliyoanza wiki tatu zilizopita.
Moshi mkali unaonekana juu ya mitaa ya mji wa Gaza uanaotoka kwenye mtambo wa umeme iliyolipuliwa wakati wa mashambulizi hayo.
Bara bara zinaonekana kuwa tupu na moshi mweusi unaonekana kutoka katika eneo la Gaza huku mitambo ya umeme ikiwa imezimwa baada ya matanki ya mafuta kupigwa.Wizara ya Afya ya Gaza imesema watu wa familia saba ni miongoni mwa wapalestina zaidi ya mia moja waliouawa katikaa eneo la mpaka baina ya Israel na Palestina uliozingirwa.

Moja kati ya familia zilizoathirika na mashambulizi hayo
Wanajeshi 10 wa Israel wameuawa siku ya Jumatatu wakiwemo wapiganaji watano wa Hamas walioingia Israel kupitia mahandaki ya chini kwa chini.
Israel inasema imegundua mahandaki ishirini na mbili ya chini kwa chini eneo la mpakani kuingia Israel yanayounganisha mtandao mpana wa mahandaki hayo.
Maafisa wa afya katika utawala wa palestina wanasema kuwa watu 60 wameuawa. Israeli inasema imeshambuliwa maeneo sitini yakiwemo makao yasiyo na mtu ya kiongozi wa kundi la Hamas Ismael Haniya na vituo vya radio na runinga vya kundi la Hamas.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa nchi yake ni lazima ijiandae kwa operesheni ya muda mrefu katika ukanda wa Gaza .
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema kuwa amesikitishwa na ripoti kuwa Israel ilisambaza ujumbe wa kuwaonya na kuwataka wenyeji kuondoka maeneo ya kaskazini mwa Gaza .
Ban amesema kuwa umoja wa mataifa hauna uwezo wa kuwasaidia watu zaidi wanaohama.

No comments:

Post a Comment