TANGAZO


Wednesday, July 2, 2014

Benki ya KCB yakabidhi vifaa vya Hospitali Kituo cha Afya Kombeni, wilaya ya Magharibi, Unguja

Wananchi waliohudhuria hafla ya kukabidhi vifaa vya Hospitali kwa kituo cha afya cha Kombeni kilichopo wilaya ya Magharibi, Unguja wakimsikiliza Meneja wa Benki ya KCB tawi la Zanzibar.
Meneja wa Benki ya KCB Tawi la Zanzibar, Sahim Abdalla Juma akiongea kwenye hafla ya kukabidhi vifaa vya hospitali ya Kituo cha Afya cha Kombeni, kilichopo wilaya ya Magharibi, Unguja. Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa vina thamani ya Sh. milioni 15.
 Meneja wa Benki ya KCB Tawi la Zanzibar akikabidhi mashine maalumu ya Infant Incubator kwa ajili ya kuhifadhia watoto ambao hawakutimia (NJITI). Vifaa hivyo vya hospitali vilikabidhiwa kwa kituo cha afya cha Kombeni kilichopo wilaya ya Magharibi, Unguja.  
Meneja wa Benki ya KCB, Tawi la Zanzibar, Sahim Abdalla Juma (kulia), akikabidhi vifaa vya Hospitali kwa kituo cha afya cha Kombeni kilichopo wilaya ya Magharibi, Unguja kwa Daktari wenye dhamana ya wilaya hiyo, Lela Salim Juma, jana.

No comments:

Post a Comment