Mtu mmoja amefariki na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulizi la bomu mjini Arusha Tanzania.
Polisi wamewakamata watu wawili wakihusishwa na
shambulio hilo lililotokea kwenye mgahawa wa 'Vama Traditional Indian
cuisine' jijini Arusha Kaskazini mwa Tanzania.Shambulizi hilo lilitokea siku ya jumatatu saa nne usiku.
Watu wasiojulikana walirusha bomu ndani ya mgahawa kupitia mlangoni ambapo watu wanane wamejeruhiwa moja kati yao akiwa na majeraha makubwa.
Polisi wanaendelea na upelelezi kuhakikisha inawatia nguvuni watu waliohusika na matukio hayo.
Haijulikani kilichosababisha mlipuko huo.
No comments:
Post a Comment