Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, TANTRADE, Bi. Jaqueline Mneney Maleko akizungumza na waandishi wa habari (hawako
pichani), Dar es Salaam leo, kuhusu Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es
Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara ya Nje wa TANTRADE, Bibi. Anna
Bulondo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, TANTRADE, Bi. Jaqueline Mneney Maleko akizungumza na waandishi wa habari (hawako
pichani), Dar es Salaam leo, kuhusu Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es
Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara ya Nje wa TANTRADE, Bibi. Anna
Bulondo. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, TANTRADE, Bi. Jaqueline Mneney Maleko akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani), Dar es Salaam leo, kuhusu Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara ya Nje wa TANTRADE, Bibi. Anna Bulondo.
Mkurugenzi wa Biashara ya Nje wa TANTRADE, Bi. Anna
Bulondo, akifafanua jambo wakati wa mkutano huo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, TANTRADE Bi. Jaqueline Mneney Maleko
UMETOLEWA mwito kwa Watanzania kuzichangamkia fursa
mbalimbali za kibiashara, zinazoletwa na Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya
Dar es Salaam, DITF ambapo Maonyesho ya
huu, yatajumuisha makampuni zaidi ya kimataifa toka nchi yatashiriki.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo
ya Biashara Tanzania, TANTRADE, Bibi
Jaqueline Mneney Maleko wakati akizungumzia maandalizi ya Maonyesho ya
38 Kimataifa ya Dar es Salaam, kwa waandishi wa Habari, ofisi za TANTRADE
jijini Dar es Salaam leo.
Bibi Maleko amesema,
lengo kuu la Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara, ni kufungua fursa za
kibiashara, kama fursa za kutafuta wabia, fursa za kutafuta wawekezaji, na fursa
za kuona bidhaa za viwango vya kimataifa ili
wazalishaji wa bidhaa za Tanzania kujitahidi kufikia viwango hivyo vya
kimataifa badala mtindo uliopo sasa kwa
watu kujitokeza kwa wingi kuja, kununua tuu bidhaa..
Maonyesho ya mwaka huu, yatashirikisha waonyeshaji bidhaa zaidi ya 1,200 kati yake
Wizara, Idara na Wakala za serikali zaidi ya 60, na makampuni zaidi ya 400 ya kimataifa
yamethibitisha kushiriki.
Bibi Maleko amesema hii ni fursa nzuri kwa Watanzania na Makampuni
ya Kitanzania kujitokeza kwa wingi na
kuchangamkia fursa zinazoambatana na maonyesho ya kimataifa.
Kauli Mbiu ya
Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam ni ni Kuunganisha Uzalishaji wa Bidhaa na
Masoko, ili kutoa fursa kwa wazalishaji wa bidhaa za Tanzania, kupata fursa za masoko ili bidhaa hizo ziweze
kukidhi vigezo vya kimataifa hivyo
kuziwezesha kuingia kwenye masoko ya
kimataifa.
Bibi Maleko, ametoa wito kwa wafanyabiashara wa Tanzania na
haswa wazalishaji bidhaa za Tanzania, ili kuweza kuingia kwenye ushindani wa
masoko ya ndani nay a kimataifa, ni muhimu kwanza ukajua mahitaji ya soko,
ndipo uzalishe bidhaa zitakazo kwenda sambamba na mahitaji na vigezo vya
masoko.
Ameeleza kama kawaida kutakuwa na banda maalum la Tanzania
lenye bidhaa za ndani zilizikidhi viwango vya kimataifa ili kuwahamasisha Watanzania kupenda bidhaa za ndani kwa kupenda
chako, jenga chako.
Pia maonyesho ya mwaka huu tayahusisha maonyresho ya
biashara za bidhaa za ubunifu na vipaji, zikiwemo bidhaa za mavazi, sanaa za maonyesho
na hata zanaa za muziki, hivyo kutakuwemo wanamuzi wataoonyesha bidhaa zao za
muziki.
Bibi Maleko ametoa
wito kwa Watanzania wasio na ajira, kuzitumia fursa za maonyesho hayo ili
waweze kujiajiri. TANTRADE itafanya kazi ya kuwajengea uwezo, wakiwemo watu
wenye makundi maalum kama wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, hivyo
TANTRADE iko kwa ajili ya kuwashika mkono, kuwanjengea uwezo, kuwatafutia
mitaji, uwezo na kuwatafutia masoko.
Bi Maloke aliwataka washiriki wote wa maonyesho hayo kufanya
maandalizi mapema na kufikia tarehe 27 ya mwezi huu, mabanda yote lazima yawe
yamemalizika, ili kukidhi viwango vya kimataifa vinavyosimamia Taasisi ya Maonyesho ya Kimataifa ya UFI.

No comments:
Post a Comment