*Wajumbe wahoji ukweli wa UKAWA kulipwa sh. 450,000 kwa siku
kwa kutohudhuria vikao vya Bunge hilo na Taasisi za Nje
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Philip Mangula akifafanua jambo mbele ya waandishi wa Habari alipowaita White House kuwaambia walichojadili Jumapili iliyopita na viongozi wa UKAWA kuhusu namna watakavyojenga maelewano katika Bunge la Katiba kilichoandaliwa na Technical Committee (TCD).
Jengo la Makao Makuu ya Chama Cha Cha Mapinduzi (CCM), lililopo katikati ya Barabara ya Tano na ya Sita Mijini Dodoma. (Picha zote na John Banda)
Jengo la Makao Makuu ya Chama Cha Cha Mapinduzi (CCM), lililopo katikati ya Barabara ya Tano na ya Sita Mijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Philip Mangula akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari alipowaita White House kuwaambia walichojadili Jumapili iliyopita na viongozi wa UKAWA.
WAJUMBE
wa Bunge la Katiba wanaounda Umoja wa Katiba ya wananchi (UKAWA),
ambao hawatahudhuria vikao vya bunge hilo, watalipwa sh. 450,000 na
taasisi za Ujerumani, zinazofadhili umoja huo, imeelezwa.
Mwenyekiti
wa kikao cha Kamati ya Ufundi ya TCD, Philip Mangula alisema suala hilo,
lilibuka katika kikao cha Kamati ya Ufundi ya TCD ambacho kilikutana leo,
ili kujadili na kupata sababu ya wanachama wa UKAWA kususia Bunge la Katiba.
"Katika kikao chetu ambacho tulikutana
Juni 8, 2014, pamoja na mambo mengine wajumbe pia walitaka kusikia kauli
ya UKAWA kuhusu tuhuma nzito zilizotolewa kwenye vyombo vya habari,
kwamba kumefanyika uchunguzi na vyombo hivyo uliobaini kuwa, yapo
mashirika mawili yanayowafadhili washiriki wa UKAWA kwa kutohudhuria
vikao vya Bunge maalum.
"Mashirika
yaliyotajwa kuwafadhili UKAWA wasihudhurie Bunge hilo ni Chama cha CDU
cha Ujerumani na Chama cha Conservative cha Uingereza.
Aidha taarifa
hizo zinaeleza kuwa taasisi ya Democratic Union Of Africa (DU-Africa),
inafadhili UKAWA.
"Taarifa
hizo zinaonesha kuwa kuwa, mwezi Machi mwaka huu UKAWA ilipokea
sh.bilioni 1.7 na baadaye ilipokea sh.380 milioni huku kuliwa na ahadi
ya kupatiwa kiasi kingine cha sh.bilioni 3.2 Baada ya kupeleka marejesho
ya matumizi ya mgawo wa kwanza." alisema Mangula.
Hata
hivyo alisema wahusika wakuu waliotakiwa kutoa ufafanuzi juu ya jambo
hilo hawakuhudhuria kikao hicho ,wajumbe wa Baraza wa kikao hicho
wamekubaliana kuitisha kikao cha Baraza la Taifa la vyama vya Siasa
linalojmuisha vyama vyote 22 vyenye usajili wa kudumu ili kuendelea
kutafakari hatma ya mchakato wa katiba wa awamu ya pili unaotarajiwa
kuanza mwezi August mwaka huu.
Aidha
Mangula aliwaambia waandishi kuwa lengo la kikao hicho lilikuwa ni
kujadiliana kwa pamoja na kujua sababu zilizowafanya baadhi ya wajumbe
waliuounda UKAWA ambao haumo katika mchakato wa uundaji wa katiba.
Alisema
hata hivyo wajumbe walishindwa kufikia azma yao kutokana na kutokuwepo
kwa wawakilishi wa vyama hivyo ili kupata maelezo fasaha ya kiini cha
tatizo lililowasukuma kususia Bunge la katiba licha ya kwamba ndani ya
kanuni za Bunge hilo kuna utaratibu uliowekwa wa kutatua matatizo na
kutoelewana kunakotokea ndani ya Bunge hilo.
"Bunge
limeweka Kamati ya maridhiano na pia Kamati ya uongozi ambazo hujadili
matatizo yatokeapo baina yao au miongoni mwa wabunge hao." alisema
Mangula
Kamati
hiyo ya Ufundi ina wawakilishi kutoka vyama vyote vinavyounda TCD
ambavyo ni CCM, Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi, TLP na UDP huku cha UPDP
kikiwakilisha vyama visivyo na wabunge.






No comments:
Post a Comment