Wafanyakazi
wa huduma za afya katika kijiji cha Mbola, mkoani Tabora wakijaribu
namna ya kutumia simu zao mara baada ya mafunzo ambapo Airtel
inawawezesha kutumia simu zao kutoa huduma za Afya chini ya mradi wa
millennium village.
Wafanyakazi wa huduma za afya katika kijiji cha Mbola, mkoani Tabora wakijaribu namna ya kutumia simu zao mara baada ya mafunzo ambapo Airtel inawawezesha kutumia simu zao kutoa huduma za Afya chini ya mradi wa millennium village.
Akitoa mafunzo kwa wafanyakazi wa huduma za afya katika kijiji cha Mbola, mkoani Tabora, namna ya kutumia huduma ya mawasiliao ya simu kutoa huduma za kiafya ambapo Airtel imewapatia wafanyakazi hao, huduma ya internet, message na simu bure na kuwawezesha kufanya kazi kwa ufanisi na kufikia maeneo mengi zaidi.
Mfanyakazi wa Huduma za Afya Bi. Amina Wakasuvi akitoa huduma kwa moja ya familia katika Kijiji cha Mbola, mkoani Tabora ambapo Airtel chini ya mradi wa millennium village imewawezesha wafanyakazi hao, kutumia mtandao wa mawasiliano kutoa huduma za Afya.
Na Mwandishi wetu, Tabora,
10 Juni 2014
WAFANYAKAZI wa Afya wa Kijiji cha Mbola, mkoni
Tabora wametoa shukrani zao kwa Airtel kufatia technologia ya huduma ya
mawasiliano inayoyowawezesha kutoa huduma za afya kwa wigo mpana na
kuwafikia wakazi wengi zaidi.
Wafanyakazi
hao wa afya walipata mafunzo ya namna ya kutumia technologia ya huduma
ya afya kupitia simu iitwayo COMCARE, iliyoanzisha kwa msaada wa Dagiba
inapatikana kupitia simu za smart phone zenye application maalumu
inayowawezesha wafanyakazi wa afya kukusanya takwimu za wagonjwa na
kutuma repoti kwenye vituo vya afya.
Akiongea
wakati wa mafunzo mmoja wa wafanyakazi wa afya Ms Amina Wakasuvi
alisema” Tekinologia hii mpya ya kisasa itatuwezesha kufatilia kazi
zinazofanywa na wafanyakazi wa afya wakiwa katika maeneo mbalimbali na
wafanyakazi hao wataweza kutuma repoti zao kwa wakati kila siku kupitia
mtandao wa Airtel.
Hivyo tunawashukuru sana Airtel kwa ubunifu huu na
huduma ya vifurushi vya internet vya bure vinavyotuwezesha kufanya kazi
zetu kwa wakati.
Akionge
wakati wa tukio hilo Meneja huduma kwa jamii Bi. Hawa Bayumi alisema”
kwa miaka mitatu sasa Airtel imewekeza katika kuleta mapinduzi ya
kupatikana kwa huduma kwa jamii husasani katika maeno ya vijiji vya
Tabora kwa kushiriki katika mradi wa Millennium village kama mtowaji
mkuu wa huduma za mawasiliano.
Katika mradi huu Airtel inatoa njia ya
mawasiliano kwa kuwezesha jamii inayoishi katika maeneo ya pembezoni
kupata huduma za Afya.
Wafanyakazi wa afya katika maeneo hayo
wameunganishwa na mtandao wa kisasa unaowapatia huduma ya internet na
simu na kurahisisha kazi zao pindi wakiwa kazini. Sasa wafanyakazi hawa
wanaweza kukusanya takwimu kwa kutumia simu na pia kuwawezesha wagonjwa
walioko vijijini kuongea na madakitari specialist walioko mjini na
kupata huduma za afya kupitia simu za mkononi”.
Bayumi
aliongeza mpaka sasa tumeiwezesha miradi mitatu kupata huduma ya kupiga
simu, ujumbe mfupi na vifurushi vya internet bure, Airtel inaendelea na
dhamira yake ya kuwaleta watanzania karibu na huduma muhimu za jamii
kupitia technologia ya mawasiliano.
Akiongea
kuhusu mradi huo, Mkurugnzi wa mradi wa Millennium Village Dk. Gerson
Nyadzi alisema “ Mtandao wa 3G wa Airtel umetuwezesha kwa kiasi kikubwa
kufikia maeneo ya vijijini ambapo huduma ni duni na haba. Kuanzia
mradi huu uanzishwe kumekuwa na ongezeko la 85% la upatikanaji wa
huduma muhimu za afya hapa Mbola. Kwa kuongeza mradi wa Child count
katika techonologia ya huduma za afya ya CommCare kutawezesha zaidi ya
wakazia 97% kupata huduma za afya kupitia watoa huduma wetu wa afya
wenye vyenzo hizi muhimu za kutendea kazi.

No comments:
Post a Comment