Watu wanaounga mkono maandamano
ya kushinikiza serikali kuwanusuru wasichana zaidi ya miambili
waliotekwa nyara na wanamgambo wa kiisilamu nchini Nigeria wamepinga
hatua ya mahakama kupiga marufuku maandamano mjini Abuja.
Polisi wametaja maandamano hayo kama tisho kwa usalama wa nchi hiyo.Kauli mbiu ya maandamano hayo ni ''Bring Back Our Girls'' yaani turejesheeni watoto wetu, na waandamanaji wanasema kuwa maandamano yao yalikuwa ya amani.
Kundi la kiisilamu la Boko Haram, limesema kuwa liko tayari kuwaachilia wasichana hao ikiwa serikali nayo itawaachilia wapiganaji wake wanaozuiliwa.
No comments:
Post a Comment