Mkulima na mkazi wa Kijiji cha Hombolo Dodoma, Wile Kaluganya akiongea jambo wakati alipokuwa akiuliza jambo kwa Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi (hayupo pichani), wakati alipowatembelea ili kusikiliza malalamiko ya madai yao wanayomdai mwekezaji wa kiwanda cha Cetawico kinachonunua zabibu za wakulima hao. (Picha zote na John Banda)
Mmoja wa wakulima wa zabibu, Joseph Sanka akiuliza jambo kwa Waziri, wakati wakulima wa zao la zabibu walipokusanyika na kutaka kujua ni lini watalipwa fedha zao sh. mil. 700, wanazomdai mwekezaji wa kiwanda cha kutengeneza wine cha Cetawico kutokana na kutowalipa fedha zao, zaidi ya milioni 700 za tangu mwaka jana.
Ofisa Tarafa wa Tarafa ya Hombolo, Isaac Songoro, kizungumza jambo mbele ya Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Dk. David Malole, Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa wa Dodoma, Hezekiah Chibulunje na viongozi wengine wa Serekali, namna muwekezaji wa kiwanda cha kutengeneza mvinyo cha Cetawico, asivyo na ushirikiano na viongozi wa Serikali.
Mhasibu wa kiwanda cha Cetawico, Jackison Temu, akimsomea idadi ya madeni wanayodai wakulima, Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi na viongozi wengine waliofika kiwandani hapo kutaka kujua ni kwa nini Mwekezaji wa kiwanda hicho, ameshindwa kuwalipa wakulima fedha zao, kwa wakati.
Baadhi ya wakulima wa zao la Zabibu wa kijiji cha Hombolo, wakiwa wamekusanyika walipokuwa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Kilimo, Godfrey Zambi aliyefika kusikiliza madai ya madeni yao kwa mwekezaji wa kiwanda cha Cetawico anayedaiwa zaidi ya sh. mil. 700 na wakulima hao.
Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi akifafanua jambo, wakati alipokuwa akizungumza na wakulima wa zao la zabibu, wanaomdai mwekezaji wa kiwanda cha Cetawico kinachowakopa zabibu zao na kushindwa kuwalipa kwa wakati ambapo kwa misimu miwili mwekezaji huyo, anadaiwa zaidi ya sh. mil. 700. Waliokaa kushoto ni Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Hezekiah Chibulunje na kulia ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Hombolo Bwawani, Jerad Mtagwa.
Na John Banda, Dodoma
WAKULIMA wa zao la zabibu katika kijiji cha Hombolo, wameitaka Serikali kuwasimamia ili waweze kulipwa madai yao, ya zaidi ya sh. milioni 700, wanazomdai mwekezaji wa kiwanda cha kutengeneza mvinyo cha Cetawico na baada ya hapo afukuzwe kutokana kuzarau wazawa.
Wakulima hao, waliofikisha malalamiko yao mbele ya Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi aliyefika katika kjiji hicho, cha Hombolo, Manispaa ya Dodoma, ili kusikiliza kilio chao.
Katibu wa Ushirika wa Wakulima wa zabibu na Masoko Hombolo, Ramadan Mkombozi, alisema wanamdai mwekezaji wa kiwanda hicho, cha Cetawico Dk. Florenzo Chesini, raia wa Italy sh. mil. 700 kwa zaidi ya miezi 9 sasa, hali inayowasababishi ugumu wa maisha kutokana na wengi wao, kushindwa kulipa mikopo.
Alisema kuwa pamoja na jitihada mbalimbali walizofanya, zikiwemo
kushirikisha Serikali ya Wilaya na Mkoa ili kuwasaidia kudai madeni yao, bado wamegonga mwamba kutokana na kutopewa ushirikiano na badala yake kuishia kupewa majibu yasiyoridhisha.
‘’Mhe. Naibu Waziri kwa kuwa umekuja, tunaweza kupata madai yetu, lakini huyu mwekezaji, hii siyo mara yake ya kwanza kutokutulipa, hata mwaka jana, msimu wa mwezi wa pili, ilibidi Waziri Chiza, aingilie kati ndio tukalipwa, japo si malipo yote, tunachoomba ni bora aondolewe ili aletwe mwingine atakayeshirikina na sisi vizuri.
Hata bei yenyewe, si nzuri kwa sababu akipekewa zabibu huwa zinapimwa, tunaziacha na bei anapanga yeye kwa Kiangazi analipa kilo moja sh 800 au 1000, wakati wa Masika sh. 500 au 400 bila kujali gharama za uendeshaji, hali inayotupa hasara mara kwa mara, na mtu akihoji anaambiwa asipeleke tena, nasi hatuna pa kupeleka kutokana na kutokuwepo na viwanda vingine’’, alisema.
Awali, Mhasibu wa kiwanda cha Cetawico, Jacson Temu alimwambia Naibu Waziri Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi aliyefika kutaka kujua kiasi wakulima hao, wanachodai kuwa ni sh. mil. 703. ambazo Mwekezaji andaiwa na wakulima.
Baada ya maelezo ya mhasibu huyo, ndipo naibu waziri huyo, alipomuagiza kumfikishia ujumbe bosi wake, kuwa ahakikishe ndani ya mwezi huu, wa sita, wakulima hao, wanalipwa fedha zao zote la sivyo Serikali itachukua hatua.
No comments:
Post a Comment