TANGAZO


Monday, June 30, 2014

Vodacom yafungua duka la 80 la huduma kwa wateja mjini Tanga

*RC Tanga awapongeza kwa huduma

Muonekano wa duka jipya la Vodacom la huduma kwa wateja lililopo Barabara ya tatu linavyoonekana muda mfupi kabla ya kuzinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Captain Mstaafu Chiku Galawa.
Mkuu wa  Mkoa wa Tanga Kapteni Mstaafu Chiku Galawa (katikati) akilizindua rasmi duka jipya la kisasa la Vodacom la huduma kwa wateja lililopo barabara ya tatu. Kulia ni Mkuu wa Mauzo ya Rejareja wa Vodacom Upendo Richard na Meneja Uhusiano wa Nje wa Kampuni hiyo Salum Mwalim (wa kwanza kushoto). Duka hilo ni la 80 kwa nchi nzima ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kampuni hiyo wa kuwahudumia wateja wake kwa karibu na kwa ubora zaidi.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Kapteni Mstaafu Chiku Galawa (kulia), akiangalia simu ya kisasa aina ya Vodafone 785 inayopatikana kwa bei ya Sh. 100,000 kwenye duka la Vodacom la huduma kwa wateja lililopo barabara ya tatu mkoani humo mud mfupi baada ya Mkuu huyo kulizindua rasmi. Wnamopatia maelezo ni Upendo Richard Mkuu wa Mauzo ya Rejareja (katikati) na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim(kushoto).
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Kapteni Mstaafu Chiku Galawa (mwenye koti jeusi) akifuatilia maelezo kutoka kwa Meneja wa Mmabo ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim (kushoto) kuhusu ubora wa huduma za Vodacom na jinsi zinavyopatikana nchi nzima muda mfuopi baada ya Mkuu huyo wa Mkoa kuzindua duka jipya la huduma kwa wateja lilipo barabara ya tatu Mkoani humo. Kalia ni Mkuu wa Idara ya Mauzo ya Rejareja wa Vodacom Upendo Richard.
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Kapteni Mstaafu Chiku Galawa (katikati) akizungumza na Maofisa wa Vodacom na wa kampuni ya Jurax Investement wakati wa uzinduzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Kapteni Mstaafu Chiku Galawa (wa tatu kushoto waliosimama) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Vodacom pamoja na kampuni ya Jurax muda mfupi baada ya Mkuu wa Mkoa kuzindua rasmi duka jipya na la kisasa la Vodacom la huduma kwa wateja lililopo Barabara ya Tatu.

WATEJA wa Vodacom mkoani Tanga sasa wanaweza kuhudumiwa kwa uharaka na ubora zaidi kufuatia kampuni ya Vodacom kufungua duka lake jipya na la kisasa la huduma kwa wateja lililopo barabara ya tatu mkoani humo.
Duka hilo ambalo ni la 80 kwa Vodacom nchi nzima limefunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Kapteni Mstaafu Chiku Galawa na kupongeza  juhudi za Vodacom za kuwaletea karibu huduma wateja wake mkoani humo.
Miongoni mwa huduma zinazopatikana kwenye duka hilo ni pamoja na utauiz w amasula ya kiufundi ikiwemo huduma ya M-pawa, mauzo ya bidhaa za simu na modemu n.k.
Awali, Vodacom ilikuwa na duka la iana hiyo lililokuwepo barabara ya 11 kabla ya kufungwa na kufunguliwa hilo jipya katika barabara ya 3 likiwa na uwezo na ubora mkubwa zaidi unaoweza kukidhi kutoa huduma kwa ufanisi zaidi tofauti na hali ilivyokuwa hapo awali.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema jamii imeona jinsi ambavyo huduma za mawasiliano zilivyo muhimu kwa maisha yao na kwa mantiki hiyo mkakati wowote wa kuboresha huduma kwenye sekta ya mawasiliano unatoa nafasi kwa sekta hiyo kutoa mchango zaidi katika maisha ya watu.
Amesema simu za mkononi zimekuwa chachu ya unafuu na maisha ya watu kubadilika wakiwa sas ana uwezo w akufanya mambo mengi zaidi kupitia simu zao za mkononi ikiwemo kupiga na kupokea simu, intaneti na huduma za kifedha.
Kampuni ya Vodacom ndio inayoongoza soko la huduma za mawasiliano ya simu za mkononi nchini ikiwa na mtandao mpana zaidi wa wateja, mtandao mpana wa huduma za kifedha kupitia M-pesa na mtandao mpana zaidi wa minara ya 3G unaotoa uwezo wa huduma za intaneti.
"Huduma za mawasiliano za simu za mkononi ni chachu ya maendeleo na ukuaji wa shughuli za  kibiashara na kijamii hilo linafahamika na liko wazi hivyo basi kuboresha huduma kwenye sekta hiyo ni jambo linawaoongezea uwezo wananchi kunufaika na huduma zenyewe."Alisema Mkuu wa Mkoa Galawa
Ameipongeza Vodacom kwa namna ambavyo imekuwa ikijitahidi kuhakikisha huduma bora za mawasiliano sehemu mbalimbaliu nchini ikiwemo mkoa wa Tanga jambo ambalo amesema linachangia kuuchangamsha mkoa huo na kulinda hadhi yake huku akitoa rai kwa Vodacom kufungua maduka mengine katika ngazi ya Wilaya.
Aidha, ameipongeza pia kampuni hiyo kuweka simu za kisasa za Smartphone na kuziuza kwa bei nafuu hatua ambayo itawasaidai wananchi wa vipato vya wastani na vya chini nao kumudu kumiliki simu hizo na kunufaika na huduma za intaneti.
"Kwa hili lazima ninwapongeze, mnafanya kazi nzuri na kubwa inayoonekana na kila mmoja ikiwemo huduma ya M-pawa ambayo inawapa watu uwezo wa kuweka akiba na kukopa na kuwa na uwezo wa kufahamu taarifa za akaunti zao mara moja wanapozihitaji.Alisema Mkuu wa Mkoa Galawa
Aliongeza "Nimwaambie tu kwamba kwa Tanga mmewekeza mahala sahihi na faida yake mtaiona kwani mkoa huu sasa umeanza kuinuka huku shughuli za biashara nazo zikiongezeka ambazo pamoja na mambo mengine zinahitaji uwepo wa huduma imara na bora za mawasiliano."
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Huduma za Mauzo ya Rejareja wa Vodacom Upendo Richard amesema kuwa kuhamishwa kwa duka hilo kutoka barabara ya 11 ni matokeo ya mpango mkakati wa Vodacom wa kuhakikisha wateja wake wanakuwa na mahala bora na salama pa kupatia huduma.
Amesema baada ya kubaini changamoto kadhaa zilizokuwa zikiwakabili wateja wa Vodacom mkoa wa Tanga kutokana na ufinyu na mahala ambapo duka la awali lilikuwepo, waliamua kulifunga na sasa wamerudi wakiwa na duka kubwa zaidi na lenye ubora na uwezo wa hali ya juu wa kuwahudumia wateja.
"Tunatambua kuwa haikuwa rahisi kwa wateja wetu kukosa duka la kuwahudumia kwa takribani miezi mitano iliyopita, yalikuwa ni maamuzi magumu lakini yaliyolenga kutoa nafasi ya maboresho makubwa. Ni wazi kwa kufungua duka hili kila mmoja ametambua kile ambacho kilikuwa ndani ya mipango yetu na kila mteja sasa atafurahia uamuzi wetu."Alisema Upendo
Upendo amesema kufunguliwa kwa duka hilo kunafikisha idadi ya maduka ya Vodacom ya huduma kwa wateja kufikia 80 kwa nchi nzima huku mipango ikiendelea kufungua maduka mengine zaidi ndani ya Mkoa wa Tanga na mikoa mengine.
Upendo amesema maduka hayo sio tu kwamba yanatoa nafasi ya wateja wa Vodacom kupata huduma bora na kwa urahisi bali pia huchochea uwekezaji katika mikoa na wilaya yanapofunguliwa huku mfumo wake wa uendeshaji kwa njia ya ubia na wafanyabiashara binafsi kunachangia kutoa fursa kwa wafanyabiashara hao kufanya akzi na Vodacom na kuvuna uzoefu.
"Maduka yetu mengi tunayaendesha kwa ubia na makampuni binafsi, hii imesaidia kuwapatia nafasi wafanyabiashara wengi wa hapa nchini kufanya biashara nasi, kukuza mitaji yao, kutengeneza ajira na kustawisha maendeleo kwenye maeneo husika."Alisema Upendo.

No comments:

Post a Comment